1Muombe Yawe awape mvua za masika.
Yawe ndiye anayeleta mawingu ya mvua;
ndiye anayewapa watu mvua za manyunyu,
na kustawisha mimea katika shamba kwa ajili ya wote.
2Sanamu zao za kupigia ramuli ni uongo mutupu,
na waaguzi wao wanaagua uongo;
watabiri wao wanatabiri ndoto danganyifu,
na kuwapa watu faraja za bure.
Ndiyo maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo;
wanataabika maana wamekosa muchungaji.
3Yawe anasema hivi:
Nimewaka hasira juu ya hao wachungaji,
nami nitawaazibu hao watawala.
Mimi Yawe wa majeshi,
nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda.
Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.
4Kwa ukoo wa Yuda kutatokea:
watawala wa kila namna,
wakubwa wenye nguvu kama jiwe kubwa la musingi,
wanaokuwa imara kama musumari wa hema,
wenye nguvu kama upinde wa vita.
5Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa katika vita,
watawakanyaga waadui zao ndani ya matope katika njia.
Watapigana kwa sababu mimi Yawe nipo pamoja nao;
nao watawafezehesha hata waaskari wapanda-farasi.
6Nitawaimarisha watu wa Yuda;
nitawaokoa wazao wa Yosefu.
Nitawarudisha kwao kwa maana ninawaonea huruma,
nao watakuwa kama vile sikuwa nimewakataa.
Mimi ni Yawe, Mungu wao,
nami nitayasikiliza maombi yao.
7Watu wa Efuraimu watakuwa kama mashujaa katika vita;
watajaa furaha kama watu waliokunywa divai.
Watoto wao wataona hayo na kufurahi,
watajaa furaha ndani ya moyo
kwa sababu yangu mimi Yawe.
8Nitawaita watu wangu
na kuwakusanya pamoja;
nimekusudia kuwakomboa,
nao watakuwa wengi kama vile mbele.
9Japo niliwatawanya kati ya mataifa,
hata hivyo, watanikumbuka wakiwa humo.
Nao pamoja na watoto wao wataishi
na kurudi katika nyumba zao.
10Nitawarudisha kutoka inchi ya Misri,
nitawakusanya kutoka Asuria;
nitawaleta katika inchi ya Gileadi na Lebanoni,
nao watajaa kila nafasi katika inchi.
11Watapitia katika bahari ya mateso,
nami nitayapiga mawimbi yake,
na vilindi vya maji ya muto Nili vitakauka.
Kiburi cha Asuria kitavunjwa
na nguvu za Misri zitatoweka.
12Mimi nitawaimarisha watu wangu,
nao watanitii na kuishi kwa kunipendeza.
Ni mimi Yawe ninayesema hivyo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.