Zaburi 44 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Maombi kwa kuomba ulinzi wa Mungu

1Kwa mukubwa wa waimbaji. Mashairi ya Wakora.

2Ee Mungu, sisi tumesikia kwa masikio yetu,

babu zetu wametuelezea

mambo uliyotenda nyakati zao,

ndiyo mambo uliyotenda hapo kale.

3Kwa mukono wako mwenyewe uliyafukuza mataifa,

na mahali pao ukawaikalisha watu wako;

uliyaazibu mataifa,

na kuwafanikisha watu wako.

4Watu wako hawakuitwaa inchi kwa silaha zao,

wala hawakupata ushindi kwa nguvu zao,

lakini kwa mukono wako mwenyewe,

kwa kuwaangazia uso wako,

maana wewe uliwapenda.

5Wewe ni mufalme wangu na Mungu wangu!

Unawajalia ushindi wazao wa Yakobo.

6Kwa nguvu yako tunawashinda waadui zetu,

kwa jina lako tunawakanyaga wanaotushambulia.

7Mimi sitegemei upinde wangu,

wala upanga wangu hauwezi kuniokoa.

8Wewe ndiwe uliyetuokoa kutoka waadui zetu;

uliwavuruga wale waliotuchukia.

9Siku zote tunakutukuza, ee Mungu;

tutakutolea shukrani kwa milele.

10Lakini sasa umetuacha na kutufezehesha;

hauendi tena na makundi yetu ya waaskari.

11Umetufanya tuwakimbie waadui zetu,

nao wakanyanganya mali zetu.

12Umetufanya kama kondoo wanaopelekwa kuchinjwa;

umetutawanya kati ya mataifa.

13Umeuzisha watu wako kwa bei ya chini;

wala haukupata faida yoyote.

14Umetupotezea heshima mbele ya jirani zetu,

nao wanatuchekelea na kutuzarau.

15Umetufanya tuzarauliwe na watu wa mataifa;

wanatutikisia vichwa vyao kwa kutusimanga.

16Muchana kutwa nimefezeheka,

na uso wangu umejaa haya tele

17kwa ajili ya maneno na mazarau ya wenye kunitukana,

kwa ajili ya waadui zangu wenye kunilipiza kisasi.

18Hayo yote yametupata sisi

ijapokuwa hatujakusahau,

wala hatujavunja agano lako.

19Hatujakuasi wewe,

wala hatujaiacha njia yako.

20Hata hivyo umetupondaponda kati ya nyama wakali;

umetuacha katika giza nzito sana.

21Tungalikuwa tumekusahau wewe Mungu wetu,

na kumukimbilia mungu wa uongo,

22ee Mungu, ungalikwisha jua jambo hilo,

kwa maana wewe unajua siri za moyo.

23Lakini kwa ajili yako tunauawa kila siku;

tunatendewa kama kondoo wa kuchinjwa.

24Amuka, ee Bwana! Mbona umelala?

Inuka! Tafazali usitutupe milele!

25Mbona unajificha mbali nasi,

na kusahau taabu na mateso yetu?

26Tumeinama mpaka katika mavumbi,

tumebanana na udongo.

27Uinuke, ukuje kutusaidia!

Utukomboe kwa sababu ya wema wako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help