1 Mambo ya Siku UTANGULIZI - Swahili Congo Revised Bible 2002
UTANGULIZIVitabu viwili vinavyoitwa “Mambo ya Siku” vinaweza kufikiriwa kama kitabu kimoja. Vyote kwa jumla ni kumbukumbu ya historia ambayo inaeleza habari za watu wa Israeli, tangu mwanzo wao mpaka wakati wa kupelekwa katika uhamisho kule Babeli. Mwanzo wa kitabu cha kwanza cha Mambo ya Siku ni hesabu ya uzao wa Waisraeli, tangu Adamu mpaka Daudi (sura 1-9). Sehemu ya pili ya kitabu, ni kusema sura 10-29, inaelekea zaidi historia ya utawala wa Daudi na kutayarisha ujenzi wa hekalu.