1Mushangilie kwa sababu ya Yawe, enyi watu wa haki!
Watu wa usawa ndio wanaostahili kumusifu Mungu.
2Mumusifu Yawe kwa zeze;
mumwimbie kwa kinubi cha nyuzi kumi.
3Mumwimbie wimbo mupya;
mupige kinubi vizuri na kushangilia.
4Neno la Yawe ni la usawa;
na matendo yake yote ni ya kuaminika.
5Yawe anapenda haki na sheria.
Dunia imejaa wema wake.
6Mbingu ziliumbwa kwa neno la Yawe,
na vyote vinavyokuwa ndani yake kwa pumzi ya kinywa chake.
7Alikusanya maji ya bahari kama katika chupa,
akavifunga vilindi vya bahari ndani ya gala.
8Dunia yote imwogope Yawe!
Wakaaji wote wa dunia wamwabudu!
9Maana alisema, na ulimwengu ukakuwa;
alitoa amri, nao ukajitokeza.
10Yawe anavunja mipango ya mataifa,
na anabadilisha mawazo yao.
11Mipango ya Yawe inadumu milele;
kusudi lake linadumu kwa vizazi vyote.
12Heri taifa ambalo Mungu wake ni Yawe;
heri wale aliowachagua kuwa watu wake mwenyewe!
13Yawe anaangalia chini kutoka mbinguni,
na kuwaona wanadamu wote.
14Kutoka kwenye kiti chake cha kifalme,
anawaangalia wakaaji wote wa dunia.
15Yeye anaunda mioyo ya watu wote,
yeye anajua kila kitu wanachofanya.
16Mufalme hawezi kuokolewa kwa kuwa na kundi kubwa;
wala shujaa hapati ushindi kwa nguvu zake kubwa.
17Farasi wa vita hafai kitu kwa kupata ushindi;
nguvu zake nyingi haziwezi kumwokoa mutu.
18Yawe anawaangalia wale wanaomwabudu,
watu ambao wanatumainia wema wake.
19Yeye anawaokoa katika kifo,
anawalinda wakati wa njaa.
20Mioyo yetu inamutumainia Yawe.
Yeye ni musaidizi wetu na ngao yetu.
21Tunafurahi kwa sababu yake;
tunatumainia jina lake takatifu.
22Wema wako ukae nasi, ee Yawe,
kwa maana tumekuwekea tumaini letu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.