Isaya 15 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Mungu ataiangamiza Moabu

1Ujumbe wa Mungu juu ya inchi ya Moabu.

Muji wa Ari katika inchi ya Moabu umeangamizwa usiku;

muji wa Kiri katika inchi ya Moabu umeangamizwa usiku.

2Watu wa Diboni wamepanda katika hekalu pahali pa juu kwa kuomboleza,

watu wa Moabu wanalia kwa ajili ya Nebo na Medeba;

vichwa vyote vimenyolewa upaa,

ndevu zao zote zimekatwa kabisa.

3Wanapita katika njia wakivaa magunia.

Kwenye paa za nyumba na viwanja vya muji

watu wanalia na kukauka kwa machozi.

4Watu wa Hesiboni na Eleale wanalia,

sauti zao zinasikilika mpaka Yasa.

Hata waaskari wa Moabu wanalia kwa sauti;

mioyo yao inatetemeka.

5Moyo wangu unaugua kwa ajili ya inchi ya Moabu;

wakimbizi wake wanakimbilia Zoari,

wanakimbia mpaka Egilati-Selisiya.

Wanapanda njia ya kwenda Luhiti wakilia,

katika njia kwenda Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.

6Kijito cha Nimurimu kimekauka;

nyasi zimekauka, majani mabichi yamenyauka,

hakuna chochote kinachoota hapo.

7Wakimbizi wanavuka kijito cha Mierebi;

wamebeba mali yao yote waliyopata,

na kila kitu walichojiwekea kama akiba.

8Kilio kimesikilika pote katika inchi ya Moabu,

maombolezo yao yamefika Eglaimu,

yamefika hata mpaka Beri-Elimu.

9Maji ya Dimoni yamejaa damu,

lakini Mungu ataongeza musiba wa Dimoni.

Hao wachache watakaobaki wazima

na kukimbia kutoka Moabu,

watapelekewa simba wa kuwaua.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help