Zaburi 142 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Maombi ya mutu aliyeachwa pekee

1Mashairi ya Daudi alipokuwa ndani ya pango.

2Ninamulilia Yawe kwa sauti kubwa,

ninamusihi Yawe kwa sauti kubwa.

3Ninamutolea malalamiko yangu,

ninamwelezea taabu zangu.

4Roho yangu inaporegea kabisa,

yeye yuko, anajua mwenendo wangu.

Waadui wamenitegea mitego katika njia ninayopita.

5Nikiangalia kwa kuume kwangu na kungojea,

ninaona hakuna mutu wa kunisaidia;

sina tena nafasi ya kukimbilia,

hakuna mutu anayenijali.

6Ninakulilia wewe, ee Yawe!

Wewe ni kimbilio langu;

wewe ni hitaji langu lote katika inchi ya wenye uzima.

7Usikilize kilio changu, maana nimetabanika sana;

uniokoe kutoka watesaji wangu, maana wamenizidi nguvu.

8Uniondoe humu katika kifungo,

kusudi nipate kukushukuru,

nikijiunga na watu wa haki

kwa sababu ya vyote ulivyonitendea.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help