Walawi 9 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Haruni anatoa sadaka

1Siku ya nane kisha siku saba za kutakaswa, Musa akamwita Haruni na wana wake pamoja na wazee wa Israeli.

2Musa akamwambia Haruni: Twaa mwana-ngombe dume kwa ajili ya sadaka ya kuondoa zambi na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, nyama wote wasikuwe na kilema. Kisha uwatoe sadaka mbele ya Yawe.

3Uwaambie Waisraeli watwae beberu mumoja kwa ajili ya sadaka ya zambi, na mwana-ngombe mumoja na mwana-kondoo mumoja wote wa umri wa mwaka mumoja na wasiokuwa na kilema kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,

4ngombe dume mumoja na kondoo dume mumoja kwa ajili ya sadaka ya amani, wamutolee Yawe sadaka pamoja na sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa maana leo Yawe atawatokea.

5Waisraeli wakaleta vyote hivyo mbele ya hema la mukutano kama vile Musa alivyowaamuru na wote pamoja wakaenda kusimama mbele ya Yawe.

6Musa akawaambia: Hili ndilo jambo ambalo Yawe aliwaamuru mulifanye kusudi utukufu wake uonekane kwenu.

7Halafu Musa akamwambia Haruni: Kwenda kwenye mazabahu, utolee pale sadaka yako kwa ajili ya zambi na sadaka ya kuteketezwa na kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili yako na kwa ajili ya watu wa Israeli. Kisha tolea pale sadaka za watu na kuwafanyia ibada ya upatanisho kama vile Yawe alivyoamuru.

8Basi, Haruni akakaribia mazabahu, akachinja yule mwana-ngombe aliyemutoa kuwa sadaka kwa ajili ya zambi yake mwenyewe.

9Wana wake wakamuletea damu, naye akachovya kidole chake katika damu hiyo na kuipakaa kwenye pembe za mazabahu. Damu iliyobakia akaimwanga kwenye tako la mazabahu.

10Lakini mafuta na figo akaviteketeza vyote juu ya mazabahu kama vile Yawe alivyomwamuru Musa.

11Lakini nyama na ngozi akaviteketeza kwa moto inje ya kambi.

12Kisha Haruni akamuchinja nyama wa sadaka ya kuteketezwa. Wana wake wakamuletea damu, naye akainyunyizia mazabahu pande zote.

13Kisha wakamuletea sadaka ya kuteketezwa, kipande kimojakimoja, na kichwa, naye akaviteketeza juu ya mazabahu.

14Akasafisha matumbotumbo na vikanyagio na kuviteketeza pamoja na ile sadaka ya kuteketezwa kwenye mazabahu.

15Kisha, Haruni akaleta mbele sadaka ya watu. Akatwaa mbuzi wa sadaka ya watu kwa ajili ya zambi, akamuchinja na kumutoa sadaka kwa ajili ya zambi, kama vile alivyofanya kwa yule wa kwanza.

16Kisha akaleta mbele ile sadaka ya kuteketezwa akatolea sadaka hiyo kulingana na agizo.

17Kisha akaleta mbele sadaka ya unga akijaza mukono mumoja na kuiteketeza juu ya mazabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya kila asubui.

18Halafu Haruni akamuchinja vilevile ngombe dume na yule kondoo dume wa sadaka za amani kwa ajili ya watu. Wana wake wakamuletea damu ambayo aliinyunyizia mazabahu pande zote. Ang. Law 3.1-11

19Mafuta ya ngombe dume huyo na kondoo dume, mukia wa kondoo, mafuta yaliyofunika matumbotumbo, figo na sehemu bora ya maini

20wakayaweka juu ya vilali, naye akaviteketeza kwenye mazabahu.

21Lakini vile vilali na ule muguu wa nyuma wa kuume, Haruni akafanya navyo kitambulisho cha kumutolea Yawe, kama vile Musa alivyoamuru.

22Haruni alipomaliza kutolea sadaka zote: sadaka kwa ajili ya zambi, sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akawainulia watu mikono, akawabariki, kisha akashuka chini. Ang. Hes 6.22-26

23Halafu Musa na Haruni wakaingia ndani ya hema la mukutano; walipotoka wakawabariki watu, nao utukufu wa Yawe ukaonekana kwa watu wote.

24Yawe akawasha moto ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya mazabahu. Watu wote walipoona huo moto wakapiga vigelegele na kuinama uso mpaka chini.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help