1Zaburi ya Asafu.
Ee Mungu,
watu wasiokujua wameshambulia inchi yako.
Wamechafua hekalu lako takatifu,
wameugeuza Yerusalema kuwa mabomoko.
2Wameacha maiti za watumishi wako zikuliwe na ndege,
wametoa miili ya watu wako kwa wanyama wa pori.
3Damu yao imemwangwa kama maji katika Yerusalema,
wamelazwa humo, wala hakuna wa kuwazika.
4Tunazarauliwa na mataifa jirani,
jirani zetu wanatuchekelea na kutusimanga.
5Ee Yawe, utakasirika hata milele?
Hasira yako itawaka kama moto hata wakati gani?
6Uyamwangie mataifa yasiyokujua hasira yako,
ndizo, tawala zote zisizoheshimu jina lako.
7Maana wamemeza wazao wa Yakobo,
wameteketeza kabisa makao ya taifa lako.
8Usituazibu kwa sababu ya makosa ya babu zetu.
Huruma yako itufikie haraka,
maana tumegandamizwa sana!
9Utusaidie, ee Mungu, mwokozi wetu
kwa utukufu wa jina lako.
Utuokoe na kutusamehe zambi zetu,
kwa ajili ya jina lako.
10Kwa nini mataifa yatuambie:
“Mungu wenu yuko wapi?”
Utujalie tuone jinsi utakavyowalipiza mataifa kisasi
kwa ajili ya mauaji ya watumishi wako.
11Kilio cha hao wafungwa kikufikie;
kwa nguvu yako kubwa uwaokoe waliohukumiwa kufa.
12Ee Bwana, uwalipize mataifa jirani mara saba
kwa ajili ya matusi waliyokutukana.
13Nasi watu wako, sisi kondoo wa kundi lako,
tutakushukuru milele,
na kukusifu nyakati zote.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.