Amosi UTANGULIZI - Swahili Congo Revised Bible 2002
UTANGULIZIAmosi aliishi mbele ya manabii wengine wote ambao tumeachiwa vitabu vyao. Yeye alizaliwa katika ufalme wa kusini wa Yuda lakini akaitwa kutumika katika ufalme wa kaskazini katika mwaka 750 mbele ya Kristo.Wakati huu ulikuwa wa fanaka na maendeleo ya uchumi na usalama. Lakini Amosi aliona kwamba hali hiyo ilipatikana kwa kutesa na kugandamiza wamasikini. Utimizaji wa mambo ya dini ulikuwa wa unafiki, na usalama wa kisiasa haukukuwa imara. Amosi alishitaki ukosefu wa haki katika taifa kwa uhodari wa pekee. Aliwaambia watu kwamba Mungu atawaazibu. Mwito wake kwa waongozi wapate kushika haki haukupokelewa vizuri. Alikatazwa kufanya kazi yake ya kinabii kule Beteli.