Zaburi 140 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Kuomba ulinzi wa Mungu

1Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi.

2Ee Yawe, uniokoe na watu wabaya,

unikinge na watesaji wakali.

3Watu hao wanafikiri mabaya siku zote,

wanaamusha ugomvi kila mara.

4Ndimi zao ni hatari kama za nyoka;

ndani ya midomo yao kuna maneno ya sumu kama ya piri.

5Ee Yawe, unilinde na makucha ya wabaya;

unikinge na watesaji wakali

ambao wamepanga kuniangusha.

6Wenye kiburi wamenitegea mitego,

wametandika kamba kama wavu,

wameficha mitego katika njia wanikamate.

7Ninamwambia Yawe: “Wewe ni Mungu wangu.”

Usikilize, ee Yawe, sauti ya ombi langu.

8Ee Yawe, Bwana wangu, mukombozi wangu mukubwa,

umenikinga salama wakati wa vita.

9Ee Yawe, usiwape waovu vitu wanavyotaka,

wala mipango yao mibaya usiifanikishe.

10Hao wanaonizunguka wanainua vichwa;

uovu wa maneno yao uwapate wao wenyewe!

11Makaa ya moto yawaangukie;

watumbukizwe katika mashimo, wasiinuke tena.

12Wanaosingizia wengine wasifanikiwe katika inchi;

uovu uwapate watesaji wakali na kuwaangamiza bila kukawia!

13Ninajua kwamba Yawe anatetea wamasikini

na kuwapatia wakosefu haki.

14Hakika watu wa haki watasifu jina lako;

watu wa usawa watakaa kwako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help