1 Mambo ya Siku 7 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Wazao wa Isakari

1Isakari alikuwa na wana wane: Tola, Pua, Yasubu na Simuroni.

2Wana wa Tola walikuwa: Usi, Refaya, Yerieli, Yamai, Ibusamu na Semweli. Hao walikuwa wakubwa wa jamaa za ukoo za Tola na watu mashujaa sana wa vita nyakati zao. Hesabu ya wazao wao siku za utawala wa mufalme Daudi ilikuwa elfu makumi mbili na mbili na mia sita.

3Mwana wa Usi alikuwa: Isirahia.

Wana wa Isirahia walikuwa: Mikaeli, Obadia, Yoeli na Isia. Wote watano walikuwa wakubwa wa jamaa.

4Kwa vile wake na watoto wao walikuwa wengi sana, walikuwa na wanaume elfu makumi tatu na sita wanaoweza kuenda kwa vita.

5Ndugu zao katika jamaa zote za kabila la Isakari walioandikwa kwa kufuata ukoo, walikuwa elfu makumi munane na saba, na wote walikuwa mashujaa wa vita.

Wazao wa Benjamina na Dani

6Benjamina alikuwa na wana watatu: Bela, Bekeri na Yediaeli.

7Bela alikuwa na wana watano: Esiboni, Usi, Usieli, Yeremoti na Iri. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa zao, na waaskari mashujaa. Walioandikwa kwa kufuata ukoo na hesabu ya wazao wao ilikuwa elfu makumi mbili na mbili na makumi tatu na wane.

8Wana wa Bekeri walikuwa: Zemira, Yoasi, Eliezeri, Eliehonai, Omuri, Yeremoti, Abiya, Anatoti na Alemeti. Wote hawa ni wazao wa Bekeri.

9Waliandikishwa kwa ukoo kulingana na vizazi vyao kama viongozi wa jamaa zao, na hesabu ya wazao wao ilikuwa elfu makumi mbili na mia mbili, wote wakiwa mashujaa wa vita.

10Mwana wa Yediaeli alikuwa: Bilihani.

Wana wa Bilihani walikuwa: Yeusi, Benjamina, Ehudu, Kenana, Zetani, Tarsisi na Ahisahari.

11Wote hawa walikuwa wakubwa wa jamaa katika ukoo zao na waaskari mashujaa wa vita. Kutokana na wazao wao, kulipatikana wanaume elfu kumi na saba na mia mbili, waaskari hodari tayari kabisa kwa vita.

12Supimu na Hupimu walikuwa wana wa Iri. Husimu alikuwa mwana wa Aheri.

Wazao wa Nafutali

13Nafutali alikuwa na wana wane: Yazieli, Guni, Yereri na Salumu. Hao walikuwa wazao wa Biliha.Wazao wa Manase

14Manase alikuwa na wana wawili kutoka kwa habara yake Mwaramu: Asirieli na Makiri. Makiri alikuwa baba ya Gileadi

15Makiri alizaa Hupimu na Supimu. Jina la dada yake lilikuwa Maka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Zolofehadi. Zolofehadi alikuwa na wabinti peke yake.

16Maka muke wa Makiri, alizaa mwana jina lake Peresi. Jina la ndugu ya Peresi lilikuwa Seresi. Wana wa Seresi walikuwa Ulamu na Rakemu.

17Rakemu alizaa Bedani. Hawa wote ni wazao wa Gileadi, mwana wa Makiri, mujukuu wa Manase.

18Hamo-Leketi, dada ya Gileadi, alizaa: Isihodi, Abiezeri na Mala.

19Wana wa Semida walikuwa: Ahiana, Sekemu, Liki na Aniamu.

Wazao wa Efuraimu

20-21Hawa ndio wazao wa Efuraimu:

Sutela alizaa Beredi,

Beredi alizaa Tahati,

Tahati alizaa Eleada,

Eleada alizaa Tohati,

Tohati alizaa Zabadi,

Zabadi alizaa Sutela.

Zaidi ya hao, Efuraimu alikuwa na wana wengine wawili, Ezeri, na Eleadi, ambao waliuawa na wenyeji wa asili wa inchi ya Gati kwa sababu walikwenda kule kuwanyanganya ngombe zao.

22Efuraimu baba yao aliomboleza vifo vyao kwa siku nyingi sana, na wandugu zake wakakuja kumufariji.

23Halafu Efuraimu akalala na muke wake, naye akapata mimba na kuzaa mwana. Efuraimu akamupa jina la Beria, kwa sababu ya magumu yaliyopata jamaa yake.

24Efuraimu alikuwa na binti jina lake Sera. Huyu ndiye aliyejenga miji ya Beti- Horoni ya juu na ya chini, na Uzeni-Sera.

25-27Efuraimu alizaa vilevile Refa,

Refa alizaa Resefi,

Resefi alizaa Tela,

Tela alizaa Tahani,

Tahani alizaa Ladani,

Ladani alizaa Amihudi,

Amihudi alizaa Elisama,

Elisama alizaa Nuni,

Nuni alizaa Yoshua.

28Inchi zao na makao yao yalikuwa: Beteli na vijiji vyake, muji wa Narani uliokuwa upande wa mashariki, muji wa Gezeri uliokuwa upande wa magaribi pamoja na vijiji vyake, Sekemu na vijiji vyake, na Aya na vijiji vyake.

29Na vilevile kwenye mipaka ya wana wa Manase: Beti-Seani na vijiji vyake, Tanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake na Dori na vijiji vyake.

Hiyo ndiyo miji ambomo wazao wa Yosefu, mwana wa Israeli walimoishi.

Wazao wa Aseri

30Wana wa Aseri walikuwa: Imuna, Isiwa, Isiwi na Beria, pamoja na binti mumoja jina lake Sera.

31Wana wa Beria walikuwa: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba ya watu wa muji wa Birza-Iti.

32Wana wa Heberi walikuwa: Yafuleti, Someri na Hotamu, na binti mumoja jina lake Sua.

33Wana wa Yafuleti walikuwa: Pasaki, Bimuhali na Asiwati.

34Wana wa Someri walikuwa: Roga, Yehuba, na Aramu.

35Wana wa Helemu walikuwa: Sofa, Imuna, Selesi na Amali.

36Wana wa Sofa walikuwa: Sua, Harneferi, Suali, Beri, Imura,

37Bezeri, Hodi, Sama, Silisa, Itirani na Bera.

38Wana wa Yeteri walikuwa: Yefune, Pisipa na Ara.

39Wana wa Ula walikuwa: Ara, Hanieli na Risia.

40Hao wote walikuwa wazao wa Aseri na walikuwa wakubwa wa jamaa zao, watu wafundi na hodari wa vita. Hesabu ya wale walioandikwa kwa kufuata ukoo katika kundi la waaskari ilikuwa elfu makumi mbili na sita.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help