Zaburi 69 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Maombolezo

1Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa wimbo “Mayungiyungi.” Zaburi ya Daudi.

2Uniokoe, ee Mungu;

maji yamenifikia katika shingo.

3Ninazama ndani ya matope mengi,

hakuna pahali pa kuweka miguu.

Nimetumbukia kwenye shimo refu la maji,

ninachukuliwa na maji mengi.

4Ninaregea kwa ajili ya kulalamika,

na koo langu limekauka.

Macho yangu yamefifia,

nikikungojea ewe Mungu wangu.

5Watu wengi kuliko nywele zangu wananichukia.

Wana nguvu sana hao wanaotaka kuniua,

hao wanaonishambulia kwa mambo ya uongo.

Nirudishe kitu ambacho sikuiba?

6Ee Mungu, unajua upumbafu wangu;

makosa yangu hayafichwi mbele yako.

7Wanaokutumainia wasifezeheke kwa sababu yangu,

ee Bwana wetu, Yawe wa majeshi;

wanaokutafuta, wasizarauliwe kwa sababu yangu,

ee Mungu wa Israeli.

8Kwa ajili yako ninavumilia matusi;

haya imefunika uso wangu.

9Nimekuwa mugeni kwa wandugu zangu,

kaka na dada zangu hawanitambui.

10Upendo wangu kwa ajili ya nyumba yako unanichoma.

Matusi wanayokutukana yananiangukia.

11Nilipojinyenyekeza kwa kufunga kula chakula,

watu walinilaumu.

12Nilipovaa gunia kwa kuomboleza,

nikageuka kuwa wimbo kwao.

13Nimekuwa kichekesho kwa watu katika barabara;

walevi wanatunga nyimbo juu yangu.

14Lakini mimi ninakuomba wewe, ee Yawe.

Ee Mungu, ukubali maombi yangu wakati unaopenda.

Kwa wingi wa wema wako unijibu.

Wewe mukombozi anayestahili kuaminiwa,

15uniokoe nisizame katika matope;

uniokoe na hao wanaonichukia,

unilinde salama kutoka shimo refu la maji.

16Usiniache nipelekwe na maji mengi,

au nizame kwenye shimo lake,

au nimezwe na kifo.

17Ee Yawe,

unijibu, unielekee,

kwa uzuri wa wema wako,

kwa wingi wa rehema yako.

18Usimugeuzie mutumishi wako mugongo,

unijibu haraka, maana niko katika hatari.

19Unisogelee karibu na kunikomboa,

uniokoe na waadui zangu wengi.

20Wewe unajua ninavyotukanwa,

unajua haya na matusi ninazopata;

na waadui zangu wote wewe unawajua.

21Matusi yamevunja moyo wangu,

nami nimekata tamaa.

Nimetafuta kitulizo lakini sikupata,

nimetafuta wa kunifariji lakini sikumupata.

22Walinipa sumu ndani ya chakula,

na nilipokuwa na kiu wakanipa divai inayochacha.

23Karamu zao zikuwe mutego kwao,

na sikukuu zao ziwanase.

24Macho yao yatiwe giza wasiweze kuona,

uikunje siku zote migongo yao.

25Uwamwangie hasira yako,

kasirani yako iwaangukie.

26Kambi zao ziachwe matongo,

mutu yeyote asiishi katika mahema yao.

27Maana wanamutesa yule uliomwazibu,

wanawaongezea maumivu wale uliowaumiza.

28Uwaazibu kwa kila uovu wao;

ukatae kabisa kuwasamehe.

29Uwafute katika kitabu cha wenye kuishi,

wasikuwe katika hesabu ya watu wa haki.

30Lakini mimi ninayekuwa muzaifu na mugonjwa,

uniinue juu, ee Mungu, uniokoe.

31Kwa wimbo nitalisifu jina la Mungu,

nitamutukuza kwa shukrani.

32Jambo hili litamupendeza Yawe zaidi,

kuliko kumutolea sadaka ya ngombe,

kuliko kumutolea ngombe dume muzima.

33Wanyenyekevu wataona hayo na kufurahi;

wanaomutafuta Mungu watapata moyo.

34Yawe anawasikiliza wakosefu;

hatawasahau hata kidogo watu wake wafungwa.

35Enyi mbingu na dunia, mumusifu Mungu;

bahari na vyote vinavyokuwa ndani yenu, mumusifu.

36Maana Mungu ataokoa Sayuni,

na kuijenga tena miji ya Yuda.

Watu wake wataishi humo na kuirizi;

37wazao wa watumishi wake watairizi,

wale wanaopenda jina lake wataishi humo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help