1Kisha, viongozi wa watu wakakaa katika Yerusalema; watu wengine wote, wakapiga kura kati ya kila jamaa kumi kwa kuchagua jamaa moja itakayokaa katika Yerusalema, muji mutakatifu. Jamaa zingine tisa zikakaa katika miji yao mingine.
2Watu wakawasifu wale wote waliokubali kukaa katika Yerusalema.
3Na katika miji mingine, watu wa Israeli, makuhani, Walawi, walinzi wa milango na wazao wa watumishi wa Solomono, walikaa katika maeneo yao wenyewe, katika miji yao.
4Watu wamoja wa kabila la Yuda na wa kabila la Benjamina walikaa katika Yerusalema:
Hawa ndio watu wa ukoo wa Yuda waliokaa Yerusalema:
Ataya mwana wa Uzia, mujukuu wa Zakaria mwana wa Amaria mwana wa Sefatia mwana wa Mahalaleli wa uzao wa Peresi;
5Maseya mwana wa Baruku mwana wa Koli-Hoze mwana wa Hazaya mwana wa Adaya mwana wa Yoyaribu mwana wa Zekaria, Mushilo.
6Wazao wote wa Peresi waliokaa katika Yerusalema walikuwa wanaume mashujaa mia ine makumi sita na wanane.
7Watu wa ukoo wa Benjamina waliokaa katika Yerusalema ni:
Salu, mwana wa Mesulamu mwana wa Yoedi mwana wa Pedaya mwana wa Kolaya mwana wa Maseya mwana wa Itieli na mwana wa Yesaya.
8Nyuma ya huyo kulikuwa Gabayi na Salayi. Jumla yao mia tisa makumi mbili na wanane.
9Yoeli mwana wa Sikiri, alikuwa ndiye mukubwa wao; naye Yuda mwana wa Hasenua alikuwa mukubwa wa pili wa muji.
10Makuhani waliokaa katika Yerusalema walikuwa:
Yedaya mwana wa Yoyaribu, Yakini,
11Seraya mwana wa Hilkia mwana wa Mesulamu mwana wa Zadoki mwana wa Merayoti mwana wa Ahitubu aliyekuwa musimamizi wa nyumba ya Mungu,
12pamoja na wandugu zao waliofanya kazi katika hekalu walikuwa mia nane makumi mbili na wawili. Pamoja na hao, kulikuwa Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia mwana wa Amsi mwana wa Zakaria mwana wa Pasuri mwana wa Malkiya;
13vilevile wandugu zake waliokuwa wakubwa wa jamaa za baba zao; wote pamoja walikuwa watu mia mbili makumi ine na wawili. Vilevile kulikuwa Amasayi, mwana wa Azareli mwana wa Azayi mwana wa Mesilemoti mwana wa Imeri,
14pamoja na wandugu zao; wote wakiwa mia moja makumi mbili na wanane, watu mashujaa. Na mukubwa wao alikuwa Zabdieli mwana wa Hagedolimu.
15Nao Walawi waliokaa katika Yerusalema walikuwa:
Semaya mwana wa Hasubu mwana wa Azirikamu mwana wa Hasabia, na mwana wa Buni.
16Sabetayi na Yozabadi, wakubwa wa ukoo wa Walawi, walikuwa wasimamizi wa kazi za inje ya nyumba ya Mungu,
17na Matania mwana wa Mika mwana wa Zabudi, wa uzao wa Asafu, aliyekuwa kiongozi wakati wa kuomba maombi ya shukrani. Bakubukia alikuwa musaidizi wake. Pamoja nao kulikuwa Abuda mwana wa Samua mwana wa Galali wa uzao wa Yedutuni.
18Walawi wote waliokaa katika Yerusalema, muji mutakatifu, walikuwa mia mbili makumi munane na wane.
19Walinzi wa milango waliokaa katika Yerusalema walikuwa:
Akubu na Talmoni pamoja na wandugu zao waliokuwa wakilinda milango, walikuwa mia moja makumi saba na wawili.
20Watu wengine wa Israeli, makuhani na Walawi walikaa katika miji ya Yuda, kila mumoja katika urizi wake.
21Lakini watumishi wa hekalu walikaa Yerusalema katika eneo la Ofeli wakiwa chini ya usimamizi wa Ziha na Gisipa.
22Kiongozi wa Walawi waliokaa Yerusalema alikuwa, Uzi, mwana wa Bani mwana wa Hasabia mwana wa Matania mwana wa Mika wa ukoo wa Asafu, waliokuwa waimbaji, viongozi waangalizi wa shuguli za nyumba ya Mungu.
23Mufalme alikuwa ametoa amri juu ya utaratibu wa kazi zao na mahitaji yao ya kila siku.
24Petahia mwana wa Mesezabeli, wa ukoo wa Zera katika kabila la Yuda, alikuwa musimamizi wa mufalme juu ya mambo yote ya watu wa Yuda.
Watu wa miji mingine25Watu wengine walikaa katika miji karibu na mashamba yao. Watu wamoja wa kabila la Yuda walikaa Kiriati-Arba, Diboni na Yekabuseli pamoja na vijiji vilivyoizunguka.
26Wengine vilevile walikaa katika miji ya Yesua, Molada, Beti-Peleti,
27Hazari-Suali na Beri-Seba pamoja na vijiji vilivyoizunguka.
28Wengine walikaa katika muji wa Ziklagi, Mekona na vijiji vilivyoizunguka.
29Wengine walikaa katika miji ya Eni-Rimoni, Sora, Yarmuti;
30Zanoa na Adulamu pamoja na vijiji vilivyoizunguka, Lakisi na mashamba yanayouzunguka, na katika Azeka pamoja na vijiji vinavyouzunguka. Hii ina maana kwamba watu wa Yuda walikaa katika eneo linalokuwa kati ya Beri-Seba upande wa kusini na Bonde la Hinomu upande wa Kaskazini.
31Watu wa kabila la Benjamina walikaa Geba, Mikimasi, Ai, Beteli na vijiji vinavyoizunguka.
32Wengine walikaa Anatoti, Nobu, Anania,
33Hazori, Rama, Gitaimu,
34Hadidi, Seboimu, Nebalati,
35Lodi na Ono lililokuwa Bonde la Wafundi.
36Walawi wamoja wa Yuda wakachanganyika na watu wa Benjamina.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.