Zaburi 92 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Wimbo wa kumusifu Mungu

1Zaburi. Wimbo wa Siku ya Sabato.

2Ni vizuri kukushukuru, ee Yawe,

kuliimbia jina lako sifa, ee Mungu Mukubwa.

3Ni vizuri kutangaza wema wako asubui,

na uaminifu wako kwa wakati wa usiku,

4kwa muziki wa zeze na kinubi,

kwa sauti tamu ya zeze.

5Ee Yawe, matendo yako makubwa yananifurahisha;

nitashangilia kwa sababu ya mambo yote uliyotenda.

6Matendo yako, ee Yawe, ni makubwa sana!

Mawazo yako hayatambulikani!

7Mutu mupumbafu hawezi kufahamu,

wala mujinga hajui jambo hili:

8kwamba waovu wanaweza kustawi kama majani,

watenda maovu wote wanaweza kufanikiwa,

lakini mwisho wao ni kuangamia milele.

9Lakini wewe, ee Yawe, ni mukubwa kwa milele.

10Hao waadui zako, ee Yawe,

hao waadui zako, hakika wataangamia;

wote wanaotenda maovu, watatawanyika!

11Wewe umenipa nguvu kama mbogo;

umenimimia mafuta kwa kunifurahia.

12Kwa macho yangu, nimeona waadui zangu wameshindwa;

kwa masikio yangu, nimesikia kilio cha wanaotenda maovu.

13Watu wa haki wanastawi kama mingazi;

wanakomaa kama mierezi ya Lebanoni!

14Kama miti iliyopandwa katika nyumba ya Yawe,

wanastawi katika viwanja vya Mungu wetu;

15inaendelea kuzaa matunda hata katika uzee;

siku zote wamejaa utomvu na wabichi,

16wapate kutangaza kwamba Yawe ni wa usawa.

Yeye ni kikingio changu.

Kwake hakuna upotovu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help