Zaburi 118 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Maombi ya shukrani

1Mumushukuru Yawe, kwa sababu ni muzuri!

Wema wake unadumu milele!

2Watu wa Israeli waseme:

“Wema wake unadumu milele.”

3Wazao wa Haruni waseme:

“Wema wake unadumu milele.”

4Wote wanaomwabudu Yawe waseme:

“Wema wake unadumu milele.”

5Katika taabu yangu nilimwomba Yawe,

naye akanisikia na kuniweka huru.

6Yawe yuko nami, siogopi kitu;

mwanadamu ataweza kunifanya nini?

7Yawe yuko nami kwa kunisaidia;

nami nitawaona waadui zangu wameshindwa.

8Afazali kumukimbilia Yawe

kuliko kumutumainia mwanadamu.

9Afazali kumukimbilia Yawe,

kuliko kuwatumainia waongozi wa dunia.

10Mataifa yote yalinizunguka,

lakini kwa jina la Yawe nikayaangamiza!

11Yalinizunguka kila upande,

lakini kwa jina la Yawe, nikayaangamiza!

12Yalinizunguka, mengi kama nyuki,

lakini yakateketea kama kichaka ndani ya moto;

kwa jina la Yawe niliyaangamiza!

13Nilishambuliwa sana karibu nishindwe,

lakini Yawe alinisaidia.

14Yawe ni nguvu yangu kubwa;

yeye mwenyewe ndiye wokovu wangu.

15Sauti za furaha ya ushindi zikasikilika

katika hema za watu wa haki:

“Mukono wa Yawe umetenda mambo makubwa!

16Mukono wa nguvu wa Yawe umeleta ushindi!

Mukono wa Yawe umetenda mambo makubwa!”

17Sitakufa.

Nitaishi

na kueleza matendo ya Yawe.

18Yawe ameniazibu sana,

lakini hakuniachilia nikufe.

19Munifungulie milango ya watu wa haki,

niingie na kumushukuru Yawe!

20Huu ndio mulango wa Yawe,

watu wa haki watapitia humo.

21Ninakushukuru, ee Yawe, kwa kunijibu;

kwa sababu wewe ni wokovu wangu.

22Jiwe lililokataliwa na wajengaji,

limekuwa sasa jiwe kubwa la musingi.

23Ni Yawe aliyefanya jambo hili,

nalo ni ajabu sana kwetu.

24Hii ndiyo siku aliyoifanya Yawe;

tushangilie na kufurahi.

25Tafazali utuokoe, ee Yawe!

Tafazali utubariki, ee Yawe!

26Abarikiwe huyu anayekuja kwa jina la Yawe!

Tunawabariki kutoka katika nyumba ya Yawe.

27Yawe ni Mungu;

yeye ametujalia mwangaza wake.

Mushike matawi katika mikono,

mukiandamana mpaka kwenye mazabahu.

28Wewe ni Mungu wangu, ninakushukuru;

ninakutukuza, ee Mungu wangu.

29Mumushukuru Yawe kwa sababu ni muzuri,

kwa maana wema wake unadumu milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help