Zaburi 35 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Kuomba musaada

1Zaburi ya Daudi.

Uwapinge, ee Yawe, hao wanaonipinga;

uwashambulie hao wanaonishambulia.

2Utwae ngao yako na kikingio chako,

uinuke ukuje kunisaidia!

3Chukua mukuki na upanga wako kwa kuwazuia wale wanaonifuata.

Uniambie mimi kwamba utaniokoa.

4Wapate haya na kuzarauliwa,

hao wanaotaka kupoteza maisha yangu!

Warudishwe nyuma na kufezeheka,

hao wanaonitafutia hasara.

5Wakuwe kama maganda yanayopeperushwa na upepo,

wakikimbizwa na malaika wa Yawe!

6Njia yao ikuwe ya giza na utelezi,

wakifukuzwa na malaika wa Yawe!

7Maana walinitegea mitego bila sababu;

walinichimbia shimo bila neno lolote.

8Maangamizi yawapate wao kwa rafla,

wanaswe katika mutego wao wenyewe,

watumbukie katika shimo lao wenyewe!

9Hivi nitamufurahia Yawe;

nitashangilia kwa sababu yeye ameniokoa.

10Nitamwambia Yawe kwa moyo wangu wote:

“Wewe, ee Yawe, hakuna anayekuwa kama wewe!

Wewe unawaokoa wamasikini kutoka makucha ya wenye nguvu,

wamasikini na wakosefu kutoka mikono ya wanyanganyi.”

11Washuhuda wakorofi wanajitokeza,

wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12Wananilipa mabaya kwa mazuri;

nami pekee nimebaki ukiwa.

13Lakini wao walipokuwa wagonjwa,

mimi nilivaa magunia kuonyesha huzuni,

nilijitesa kwa kufunga kula chakula.

Niliomba nikikuwa nimeinamisha kichwa.

14Nikakuwa kama ninamulilia rafiki au ndugu yangu.

Nilikwenda huku na huko kwa huzuni,

kama mutu anayeomboleza kifo cha mama yake.

15Lakini mimi nilipoanguka,

walikusanyika kunisimanga.

Walikusanyika kuniuzi.

Wageni nisiowajua walinizomea bila kukoma,

wala hakuna aliyewazuia.

16Walinichekelea,

walinisagia meno.

17Ee Yawe, utaangalia tu mpaka wakati gani?

Uniokoe kutoka mashambulio yao;

uokoe maisha yangu kutoka simba wakali hao.

18Hivi nitakushukuru kati ya kusanyiko kubwa la watu;

nitakutukuza kati ya kundi kubwa la watu.

19Usiwaache waadui hao wabaya wanisimange,

hao wanaonichukia bure, wafurahie mateso yangu.

20Hawasemi vizuri juu ya wengine,

wanatunga tu uongo juu ya wanainchi watulivu.

21Wananishitaki kwa sauti, wakisema:

“Sawa! Sawa! Tumeona wenyewe uliyotenda!”

22Lakini wewe Yawe unaona jambo hilo.

Usinyamaze, ee Yawe,

usikae mbali nami.

23Uinuke, ee Yawe, unitetee;

ukuje, ee Mungu wangu, uangalie maneno yangu.

24Ee Yawe, Mungu wangu, unitetee,

unitendee kulingana na haki yako.

Usiwaache waadui zangu wanisimange.

25Usiwaache waseme: “Tumefanikiwa sawa tulivyotaka!”

au waseme: “Tumemumaliza huyu!”

26Uwaache hao wanaofurahia hasara yangu,

washindwe wote na kufezeheka.

Hao wote wanaojiona bora kuliko mimi,

wapate haya na kufezeheka.

27Lakini wanaotaka kuona kwamba sina kosa,

wakuwe na furaha tele, waseme siku zote:

“Yawe ni mukubwa!

Anapendezwa na kumupatia mutumishi wake uheri.”

28Hivi nitatangaza haki yako;

nitasema sifa zako muchana kutwa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help