Zaburi 93 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Mungu mufalme

1Yawe anatawala;

amejifunika utukufu mukubwa!

Yawe amevaa utukufu na nguvu!

Ameimarisha ulimwengu, hautatikisika hata kidogo.

2Kiti chako cha kifalme ni imara tangu zamani;

wewe umekuwa mbele ya nyakati zote.

3Ee Yawe, bahari zimetoa sauti;

zimenyanyua sauti zao,

bahari zinanyanyua tena uvumi wao.

4Yawe ana mamlaka juu mbinguni,

ana nguvu kuliko mulio wa bahari,

ana nguvu kuliko mawimbi ya maji.

5Ee Yawe, maagizo yako ni imara;

nyumba yako ni takatifu milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help