2 Mambo ya Siku 5 - Swahili Congo Revised Bible 2002

1Basi, Solomono akamaliza kazi zote zilizoelekea nyumba ya Yawe. Kisha Solomono akaleta mali yote baba yake Daudi aliyokuwa ameitoa kwa Mungu, ni kusema: feza, zahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mungu. Sanduku la Ageno linaletwa ndani ya hekalu(1 Fal 8.1-9)

2Basi mufalme Solomono akawakusanya kule Yerusalema wazee na viongozi wote wa makabila wa ukoo za Waisraeli kusudi waondoe Sanduku la Agano la Yawe kutoka katika muji wa Daudi, ni kusema Sayuni.

11Kisha makuhani wakatoka pale Pahali Patakatifu, kwa sababu makuhani wote waliokuwa pale bila kujali makundi yao, walikuwa wamejitakasa.

12Walawi wote waimbaji, pamoja na Asafu, Hemani, na Yedutuni, pamoja na Walawi wengine wa ukoo zao, wakiwa wamevaa nguo zao za kitani safi nao wakabeba matoazi, vinanda na vinubi, walisimama upande wa mashariki wa mazabahu. Makuhani mia moja na makumi mbili wapiga baragumu walikuwa pamoja nao.

13Waimbaji na wapiga baragumu wote pamoja walitoa sauti kwa pamoja na matoazi na vyombo vingine vya muziki, wakimusifu Yawe wakiimba: “Yeye ni muzuri. Wema wake unadumu milele.” Wakati ule nyumba ya Yawe ikajazwa na wingu. Ang. 1 Sik 16.34; 2 Sik 7.3; Ezra 3.11; Zab 100.5; 106.1; 116.1; 136.1; Yer 33.11 Ang. Kut 40.34-35

14Nao makuhani walishindwa kutumika kwa sababu ya wingu lile, maana utukufu wa Yawe ulijaza nyumba ya Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help