Zaburi 136 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Wimbo wa shukrani

1Mumushukuru Yawe kwa sababu yeye ni muzuri!

Wema wake unadumu milele!

2Mumushukuru Mungu wa miungu.

Wema wake unadumu milele.

3Mumushukuru Bwana wa wabwana.

Wema wake unadumu milele.

4Yeye peke yake anatenda miujiza mikubwa.

Wema wake unadumu milele.

5Aliumba mbingu kwa hekima.

Wema wake unadumu milele.

6Alitengeneza inchi juu ya vilindi vya maji.

Wema wake unadumu milele.

7Aliumba jua, mwezi na nyota.

Wema wake unadumu milele.

8Aliumba jua litawale muchana.

Wema wake unadumu milele.

9Aliumba mwezi na nyota vitawale usiku.

Wema wake unadumu milele.

10Aliwaua wazaliwa wa kwanza wa Misri.

Wema wake unadumu milele.

11Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko.

Wema wake unadumu milele.

12Akawaondoa kwa mukono wake wenye nguvu na mamlaka.

Wema wake unadumu milele.

13Aligawanya bahari Nyekundu katika sehemu mbili.

Wema wake unadumu milele.

14Akawapitisha watu wa Israeli humo.

Wema wake unadumu milele.

15Lakini akazamisha mufalme wa Misri na waaskari wake humo.

Wema wake unadumu milele.

16Aliongoza watu wake katika jangwa.

Wema wake unadumu milele.

17Alipiga wafalme wenye nguvu.

Wema wake unadumu milele.

18Akaua wafalme wenye utukufu.

Wema wake unadumu milele.

19Akamwua Sihoni, mufalme wa Waamori.

Wema wake unadumu milele.

20Akamwua Ogi, mufalme wa Basani.

Wema wake unadumu milele.

21Akakamata inchi zao kuwa urizi wa watu wake.

Wema wake unadumu milele.

22Ni urizi wa Israeli, mutumishi wake.

Wema wake unadumu milele.

23Alitukumbuka wakati wa uzaifu wetu.

Wema wake unadumu milele.

24Akatuokoa kutoka waadui zetu.

Wema wake unadumu milele.

25Anapatia kila kiumbe chenye uzima chakula.

Wema wake unadumu milele.

26Mumushukuru Mungu wa mbinguni.

Wema wake unadumu milele!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help