Hesabu 33 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Safari kutoka Misri mpaka Moabu

1Hivi ndivyo vituo ambavyo Waisraeli wakapiga kambi walipotoka Misri wakiwa katika makundi ya makabila yao chini ya uongozi wa Musa na Haruni.

2Musa aliandika jina la kila pahali walipopiga kambi, kituo kwa kituo, kwa agizo la Yawe.

3Waisraeli wakaondoka katika muji wa Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku moja nyuma ya Pasaka ya kwanza. Wakaondoka kwa uhodari mukubwa mbele ya Wamisri wote,

4ambao walikuwa wanazika wazaliwa wao wa kwanza wanaume Yawe aliowaua; maana Yawe alikuwa ameiazibu hata miungu yao.

5Basi, Waisraeli wakaondoka Ramesesi, wakapiga kambi yao huko Sukoti.

6Kutoka Sukoti, wakapiga kambi yao huko Etamu, kwenye ukingo wa jangwa.

7Kutoka Etamu, waligeuka na kurudi mpaka Pi-Hahiroti, upande wa mashariki wa Bali-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migidoli.

8Wakaondoka Pi-Hahiroti, wakapita bahari Nyekundu mpaka jangwa la Etamu; wakasafiri katika jangwa mwendo wa siku tatu, wakapiga kambi yao Mara.

9Kutoka Mara, wakasafiri mpaka Elimu; huko Elimu kulikuwa na chemichemi kumi na mbili za maji na mingazi makumi saba, wakapiga kambi yao pahali pale.

10Wakasafiri kutoka Elimu, wakapiga kambi yao karibu na bahari ya Nyekundu.

11Kutoka bahari Nyekundu wakapiga kambi yao katika jangwa la Sini.

12Kutoka jangwa la Sini, wakapiga kambi yao Dofuka.

13Kutoka Dofuka wakapiga kambi yao huko Alusi.

14Kutoka Alusi wakapiga kambi yao huko Refidimu, ambapo hapakukuwa maji ya kunywa.

15Wakaondoka Refidimu wakapiga kambi yao katika jangwa la Sinai.

16Kutoka Sinai wakapiga kambi yao huko Kibroti-Hatawa.

17Kutoka Kibroti-Hatawa, wakapiga kambi yao huko Haseroti.

18Kutoka Haseroti, wakapiga kambi yao huko Ritima.

19Kutoka Ritima, wakapiga kambi yao huko Rimoni-Perezi.

20Kutoka Rimoni-Perezi, wakapiga kambi yao huko Libuna.

21Kutoka Libuna wakapiga kambi yao Risa.

22Waliondoka Risa, wakapiga kambi yao huko Kehelata.

23Kutoka Kehelata, wakapiga kambi yao kwenye mulima Seferi.

24Kutoka mulima Seferi wakapiga kambi yao huko Harada.

25Kutoka Harada, wakapiga kambi yao huko Makeloti.

26Kutoka Makeloti, wakapiga kambi yao huko Tahati.

27Kutoka Tahati wakapiga kambi yao Tera.

28Kutoka Tera wakapiga kambi yao Mitika.

29Kutoka Mitika, wakapiga kambi yao Hasimona.

30Kutoka Hasimona, wakapiga kambi yao Musaroti.

31Kutoka Musaroti, wakapiga kambi yao Bene-Yaakani.

32Kutoka Bene-Yaakani, wakapiga kambi yao Hori-Hagidigadi.

33Kutoka Hori-Hagidigadi, wakapiga kambi yao Yotibata.

34Kutoka Yotibata, wakapiga kambi yao Abarona.

35Kutoka Abarona, wakapiga kambi yao Esioni-Geberi.

36Waliondoka Esioni-Geberi, wakasafiri na kupiga kambi yao katika jangwa la Sini, ni kusema Kadesi.

37Kutoka Kadesi, wakapiga kambi yao juu ya mulima Hori, kwenye mupaka wa inchi ya Edomu.

38Kwa agizo la Yawe kuhani Haruni akapanda juu ya mulima Hori, na huko, akakufa katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa makumi ine tangu Waisraeli walipotoka katika inchi ya Misri. Ang. Hes 20.22-28; Kumb 10.6; 32.50

39Haruni alikuwa na umri wa miaka mia moja makumi mbili na mitatu alipokufa juu ya mulima Hori.

40Mufalme wa Aradi, Mukanana, aliyekaa Negebu katika inchi ya Kanana akapata habari kwamba Waisraeli walikuwa wanakuja.

41Kutoka mulima Hori, Waisraeli wakapiga kambi yao Salmona.

42Kutoka Salmona, wakapiga kambi yao Punoni.

43Kutoka Punoni, wakapiga kambi yao Oboti.

44Kutoka Oboti, wakapiga kambi yao Iye-Abarimu, katika eneo la Moabu.

45Kutoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi yao Diboni-Gadi.

46Kutoka Diboni-Gadi, wakasafiri na kupiga kambi yao Almoni-Diblataimu.

47Kutoka Almoni-Diblataimu, wakasafiri na kupiga kambi yao katika milima ya Abarimu, karibu na mulima Nebo.

48Kutoka milima ya Abarimu, wakasafiri na kupiga kambi yao katika mabonde ya Moabu ngambo ya muto Yordani karibu na Yeriko.

49Wakapiga kambi hiyo karibu na muto Yordani kati ya Beti-Yesimoti na bonde la Abeli-Sitimu kwenye mabonde ya Moabu.

50Katika mabonde ya Moabu, ngambo ya muto Yordani karibu na Yeriko, Yawe akamwambia Musa:

51Uwaambie Waisraeli kwamba mutakapovuka muto Yordani na kuingia katika inchi ya Kanana,

52muwafukuze wenyeji wote wa inchi hiyo mbele yenu. Mutaziharibu sanamu zao zote za mawe na za kuyeyushwa na kubomoa kila pahali pao pa ibada.

53Mutatwaa inchi hiyo na kukaa mule kwa sababu nimewapa muirizi.

54Mutagawanya inchi hiyo kwa kura kufuata jamaa zenu; eneo kubwa kwa kabila kubwa na eneo dogo kwa kabila dogo. Ang. Hes 26.54-56

55Lakini kama musipowafukuza wenyeji wa inchi hiyo kwanza, basi wale mutakaowaacha watakuwa kama vile sindano ndani ya macho yenu au miiba kila upande, na watawasumbua.

56Nami nitawafanya ninyi kama vile nilivyokusudia kuwafanya wao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help