Zaburi 66 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Wimbo wa shukrani

1Kwa mukubwa wa waimbaji. Wimbo. Zaburi.

Enyi wakaaji wote wa dunia, mumushangilie Mungu!

2Muimbe kwa ajili ya utukufu wa jina lake,

mumusifu kwa utukufu!

3Mumwambie Mungu: “Matendo yako ni ya ajabu!

Kwa nguvu yako kubwa waadui zako wanaishiwa nguvu.

4Dunia yote inakuabudu;

watu wote wanakuimbia sifa!”

5Mukuje muone mambo Mungu aliyotenda;

ametenda mambo ya kutisha kati ya watu.

6Aligeuza bahari kuwa inchi kavu,

watu wakapita humo kwa miguu;

kwa hiyo nasi tukashangilia.

7Anatawala milele kwa nguvu yake kubwa;

macho yake yanachungulia mataifa yote.

Mwasi yeyote asisubutu kumupinga.

8Mumusifu Mungu wetu, enyi mataifa yote;

mutangaze sifa zake zipate kusikilika.

9Yeye ametujalia maisha,

wala hakutuacha tuanguke.

10Umetupima, ee Mungu,

umetujaribu kama madini kwa moto.

11Umetunasa katika wavu;

umetubebesha muzigo muzito.

12Umewaacha watu watukanyage;

tumepitia katika moto na katika maji.

Lakini sasa umetuleta kwenye usalama.

13Nitakuja ndani ya nyumba yako na sadaka za kuteketezwa,

nitakutimizia viapo vyangu

14nilivyotamka na kukuahidia mimi mwenyewe

nilipokuwa katika taabu.

15Nitakutolea sadaka za kuteketezwa za nyama wenye kunona,

sadaka za kuteketezwa za kondoo dume;

nitatoa sadaka za ngombe dume na beberu.

16Enyi munaomwabudu Mungu, mukuje wote musikilize,

nami nitawaelezea mambo aliyonitendea.

17Mimi nilimulilia kwa sauti,

sifa zake nikazitangaza.

18Kama ningalikusudia maovu ndani ya moyo,

Yawe hangalinisikiliza.

19Lakini kweli Mungu amenisikiliza;

amesikiliza maneno ya maombi yangu.

20Mungu asifiwe!

Hakukataa maombi yangu,

wala hakuacha kunitendea mema.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help