1Haleluia!
Nitamushukuru Yawe kwa moyo wangu wote,
katika mukutano wa watu wa usawa.
2Matendo ya Yawe ni makubwa sana!
Wote wanaoyafurahia wanayachunguza.
3Kila anachofanya kimejaa utukufu na heshima;
haki yake inadumu milele.
4Amesababisha matendo yake ya ajabu yakumbukwe;
Yawe ni mwenye huruma na rehema.
5Anawapa chakula wenye kumwabudu;
hasahau hata kidogo agano lake.
6Amewaonyesha watu wake nguvu ya matendo yake,
amewapa inchi za mataifa mengine zikuwe mali yao.
7Matendo yake ni ya haki na ya kuaminika;
kanuni zake zote ni za kutegemewa siku zote.
8Amri zake zinadumu milele;
zimetolewa kwa uaminifu na usawa.
9Aliwakomboa watu wake
na kufanya nao agano la milele.
Yeye ni mutakatifu na wa kutisha sana!
10Kumwogopa Yawe ni musingi wa hekima;
wote wanaotii amri zake wanajaliwa akili.
Sifa zake zinadumu milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.