Zaburi 141 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Hatari za tamaa mbaya

1Kwa mukubwa wa waimbaji: Zaburi ya Daudi.

Ninakulilia, ee Yawe,

ukuje haraka kunisaidia!

Usikilize sauti yangu wakati ninapokuita!

2Upokee maombi yangu kama ubani;

ninapoinua mikono yangu kwako, unikubali kama sadaka ya magaribi.

3Ee Yawe, ulinde kinywa changu,

uweke mulinzi kwenye mulango wa kinywa changu.

4Unikinge nisielekee kufanya mabaya,

nisijishugulishe na matendo maovu,

nisijiunge na watu wanaotenda mabaya,

wala nisishiriki hata kidogo katika karamu zao.

5Afazali mutu mwema anipige kwa kunionya;

lakini sikubali hata kidogo kusifiwa na wabaya,

maana ninaomba siku zote juu ya maovu yao.

6Wakubwa wao watakapopondwa juu ya mawe,

ndipo watatambua kwamba maneno yangu yalikuwa mazuri.

7Mifupa yao itatawanywa kwenye midomo ya kuzimu

kama kuni zilizopasuliwa vipandevipande!

8Lakini mimi ninakutegemea, ee Yawe, Mungu wangu;

ninakimbilia kwako, usiniache katika hatari.

9Unikinge na mitego waliyonitegea,

uniepushe na wavu wa hao watu waovu.

10Waovu wanaswe katika mitego yao wenyewe,

wakati mimi ninaponyoka.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help