1Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi.
2Mpaka wakati gani, ee Yawe,
utaendelea kunisahau?
Mpaka wakati gani utanificha uso wako?
3Mpaka wakati gani
nitakuwa na wasiwasi katika roho
na sikitiko katika moyo siku hata siku?
Mpaka wakati gani waadui zangu watanishinda?
4Uniangalie na kunijibu, ee Yawe, Mungu wangu.
Uyaangazie macho yangu, nisipatwe na usingizi wa kifo.
5Usiwaache waadui zangu waseme: “Tumemushinda huyu!”
Watesaji wangu wasifurahie kuanguka kwangu.
6Lakini mimi ninatumainia wema wako,
moyo wangu ufurahie wokovu wako.
Nitakuimbia wewe, ee Yawe,
kwa vyote ulivyonitendea!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.