1Maombi ya Daudi.
Ee Yawe,
usikie ombi langu la haki,
usikilize kilio changu,
uyategee sikio maombi yangu yasiyokuwa ya udanganyifu.
2Haki yangu ikuje kutoka kwako,
maana wewe unajua jambo la haki.
3Wewe unajua kabisa moyo wangu;
umenifikia usiku kunichunguza,
umenitia katika majaribu;
haukuona uovu ndani yangu,
sikusema kitu kisichofaa.
4Juu ya matendo watu wanayotenda,
mimi nimetii amri yako,
sikushika njia za watesaji wakali.
5Nimefuata siku zote njia yako;
wala sijatereza hata kidogo.
6Ee Mungu, ninakuita, maana wewe unanijibu;
unitegee sikio, uyasikie maneno yangu.
7Onyesha wema wako wa ajabu;
uwaokoe kutoka waadui zao wale wanaokimbilia kwako.
8Unilinde kama mboni ya jicho lako;
unifiche chini ya kivuli cha mabawa yako,
9mbali na mashambulio ya waovu,
mbali na waadui zangu wa hatari wanaonizunguka.
10Hao hawana huruma yoyote ndani ya moyo;
wamejaa maneno ya kujivuna.
11Wananifuatilia na kunizunguka;
wananivizia waniangushe chini.
12Wako tayari kunirarua kama simba,
kama simba mukali anavyovizia nyama.
13Ee Yawe,
simama sasa uwapiganishe na kuwaporomosha!
Kwa upanga wako uokoe nafsi yangu kutoka waovu.
14Ee Yawe, mukono wako uwafukuze kati ya watu,
tukio lao likuwe kutengana na wanaokuwa wazima.
Uwashibishe kwa akiba uliyowawekea,
watoto wao nao washibe na kuacha sehemu,
wawaachie hata na wajukuu wao.
15Lakini mimi nitauona uso wako, maana mimi ni mutu wa haki;
nitakapoamuka nitajaa furaha kwa sababu unanitokea.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.