1Mbuga na inchi kavu vitachangamuka,
jangwa litafurahi na kuchanua maua.
2Litachanua maua kwa wingi kama waridi,
litashangilia na kuimba kwa furaha.
Mungu atalijalia utukufu wa milima ya Lebanoni,
uzuri wa mulima Karmeli na wa bonde la Saroni.
Watu watauona utukufu wa Yawe,
watauona ukubwa wa Mungu wetu.
3Muimarishe mikono zaifu,
mukaze magoti yanayoregea.
4Muwaambie waliovunjika moyo:
Mujipe moyo, musiogope!
Muangalie Mungu wenu atakuja kulipiza kisasi,
atakuja kuwaazibu waadui zenu;
atakuja yeye mwenyewe kuwaokoa ninyi.
5Hapo vipofu wataona tena,
na viziwi watasikia tena.
6Viwete watarukaruka kama paa,
na bubu wataimba kwa furaha.
Maji yatabubujika katika jangwa
na vijito katika mbuga.
7Muchanga wa moto katika jangwa utakuwa ziwa la maji,
inchi kavu itabubujika vijito.
Makao ya imbwa wa pori yatajaa maji;
nyasi zitaota na kukomaa kama mianzi.
8Humo kutakuwa barabara kubwa,
nayo itaitwa Njia Takatifu.
Watu wachafu hawatapitia humo,
lakini wale watu wa Mungu tu;
wapumbafu hawatakanyaga ndani yake,
9humo hamutakuwa simba,
nyama yeyote mukali hatapitia humo,
hao hawatapatikana humo.
Lakini waliokombolewa ndio watakaopita humo.
10Waliokombolewa na Yawe watarudi,
watakuja Sayuni wakipiga vigelegele.
Watakuwa wenye furaha ya milele,
watajaliwa furaha na shangwe;
huzuni na kilio vitatoweka kabisa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.