1Zaburi ya Daudi.
Ee Yawe,
unitetee,
maana nimeishi katika ukamilifu,
nimekutumainia wewe bila kusita.
2Unijaribu, ee Yawe, na kunipima;
uchunguze moyo wangu na akili yangu.
3Wema wako uko mbele ya macho yangu,
ninaishi kutokana na uaminifu wako.
4Sikusanyiki na watu wapotovu;
sishirikiani na watu wanafiki.
5Ninachukia mikutano ya wabaya;
wala sitakusanyika na waovu.
6Ninanawa mikono yangu kuonyesha kama sina kosa,
na kuizunguka mazabahu yako, ee Yawe,
7nikiimba wimbo wa shukrani,
na kueleza matendo yako ya ajabu.
8Ee Yawe, ninapenda makao yako,
pahali utukufu wako unapokaa.
9Usiniangamize pamoja na wenye zambi,
wala usinitupe pamoja na wauaji,
10watu ambao matendo yao ni maovu kila wakati,
watu ambao wanapokea kituliro kila wakati.
11Lakini mimi ninaishi katika ukamilifu;
unihurumie na kunikomboa.
12Mimi nimesimama pahali penye kuwa imara;
nitamusifu Yawe katika kusanyiko kubwa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.