Zaburi 107 - Swahili Congo Revised Bible 2002

SEHEMU YA TANO(Zaburi 107–150)Sifa kwa Mungu mwema

1Mumushukuru Yawe kwa sababu ni muzuri!

Wema wake unadumu milele!

2Museme hivyo, enyi muliokombolewa na Yawe,

watu ambao aliwaokoa katika taabu,

3akawakusanya kutoka inchi za kigeni:

kutoka mashariki na magaribi,

kutoka kaskazini na kusini.

4Wamoja walitangatanga katika jangwa tupu,

hawakuweza kufikia katika muji wa kukaa.

5Walisikia njaa na kiu;

wakavunjika moyo kabisa.

6Halafu katika taabu yao

wakamulilia Yawe,

naye akawaokoa

katika mateso yao.

7Aliwaongoza katika njia iliyonyooka,

mpaka wakafika katika muji wa kukaa.

8Mumushukuru Yawe

kwa wema wake

na maajabu yake

kwa wanadamu.

9Yeye anakunywesha wenye kiu;

na anashibisha wenye njaa mazuri.

10Wengine waliishi katika giza na ukiwa,

wafungwa katika mateso na minyororo,

11kwa sababu waliasi maagizo ya Mungu,

na kuzarau mashauri ya Mungu Mukubwa.

12Walikuwa tabani kwa kazi ngumu,

wakaanguka chini, wala hawakuwa na wa kuwasaidia.

13Halafu katika taabu yao

wakamulilia Yawe,

naye akawaokoa

katika mateso yao.

14Aliwatoa katika giza na ukiwa,

na minyororo yao akaivunjavunja.

15Mumushukuru Yawe

kwa wema wake

na maajabu yake

kwa wanadamu.

16Yeye anavunja na kufungua milango ya shaba,

na kukatakata vifungio vya chuma.

17Wengine walipumbazika kwa sababu ya zambi zao,

waliteseka kwa sababu ya uovu wao;

18walichukizwa na chakula,

walikuwa karibu kufa.

19Halafu katika taabu yao

wakamulilia Yawe,

naye akawaokoa

katika mateso yao.

20Kwa neno lake aliwaponyesha,

akawaokoa wasiangamie.

21Mumushukuru Yawe

kwa wema wake

na maajabu yake

kwa wanadamu.

22Wamutolee sadaka za shukrani;

waeleze matendo yake kwa nyimbo za shangwe.

23Wengine walisafiri katika bahari ndani ya mashua,

na kufanya shuguli zao humo juu ya bahari.

24Waliona matendo ya Yawe,

mambo ya ajabu aliyotenda huko.

25Aliamuru, akavumisha zoruba kali,

ikarusha juu mawimbi ya bahari.

26Walitupwa juu angani, kisha chini ndani ya shimo;

uhodari wao ukawaishia katika tukio lile.

27Waliyumbayumba na kuwayawaya kama walevi;

ufundi wao ukawaishia.

28Halafu katika taabu yao

wakamulilia Yawe,

naye akawaokoa

katika mateso yao.

29Alituliza ile zoruba kali,

nayo mawimbi yakanyamaza.

30Hapo wakafurahi kwa kupata utulivu;

akawafikisha kwenye kivuko walichokiendea.

31Mumushukuru Yawe

kwa wema wake

na maajabu yake

kwa wanadamu.

32Mumutukuze katika mukutano wa watu,

na kumusifu katika baraza la wazee.

33Mungu aligeuza mito kuwa jangwa,

chemichemi akazikausha kabisa.

34Udongo wenye mboleo akaugeuza kuwa udongo usioweza kutoa,

kwa sababu ya uovu wa wakaaji wake.

35Aligeuza jangwa kuwa ziwa,

na inchi ya kukauka kuwa chemichemi za maji.

36Akawahamishia wenye njaa kule,

nao wakajenga muji wa kukaa humo.

37Walilima mashamba na kupanda mizabibu,

wakavuna mazao kwa wingi.

38Aliwabariki watu wake, wakaongezeka;

na hesabu ya wanyama wao akaizidisha.

39Kisha walipopunguka na kuwa wazaifu,

kwa kugandamizwa, kuteswa na huzuni,

40aliwazarau wakubwa waliowatesa,

akawazungusha katika jangwa lisilokuwa na njia.

41Lakini aliwaokoa wakosefu katika taabu zao,

akaongeza jamaa zao kama kundi la kondoo.

42Watu wa usawa wanapoona jambo hilo wanafurahi,

lakini waovu wote wananyamazishwa.

43Wenye hekima wafikiri juu ya mambo haya,

watambue wema wa Yawe.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help