Zaburi 122 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Sifa za Yerusalema

1Wimbo wa Safari za kidini. Wa Daudi.

Nilifurahi waliponiambia:

“Twende kwenye nyumba ya Yawe.”

2Sasa tuko tumesimama

kwenye milango yako, ee Yerusalema!

3Yerusalema ni muji uliojengwa

kusudi makundi ya watu yakutane humo.

4Humo ndimo makabila yanamofika,

ndiyo, makabila ya Yawe,

kwa kumushukuru Yawe kama Waisraeli walivyoagiza.

5Humo kulikuwa viti vya kifalme kwa kuamua maneno,

ndivyo viti vya ukoo wa Daudi.

6Muuombee Yerusalema amani mukisema:

“Wote wanaokupenda wakae katika amani!

7Ndani ya kuta zinazokuzunguka kuwe amani,

nao usalama ukuwe ndani ya nyumba zako nzuri!”

8Kwa ajili ya jamaa na wandugu zangu,

ee Yerusalema, ninakutakia amani!

9Kwa ajili ya nyumba ya Yawe, Mungu wetu,

ninakuombea upate uheri!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help