1 Mambo ya Siku 6 - Swahili Congo Revised Bible 2002

1Lawi alikuwa na wana watatu: Gersoni, Kohati na Merari.

2Wana wa Gersoni walikuwa: Libuni na Simei.

Wana wa Kohati walikuwa:

3Amuramu, Izihari, Hebroni na Usieli.

Wana wa Merari walikuwa:

4Mali na Musi.

Hawa ndio wazao wa Lawi kufuatana na babu zao:

5-6Uzao wa Gersoni:

Gersoni alizaa Libuni,

Libuni alizaa Yahati,

Yahati alizaa Zima,

Zima alizaa Yoa,

Yoa alizaa Ido,

Ido alizaa Zera,

Zera alizaa Yeaterai.

7-9Uzao wa Kohati:

Kohati alizaa Aminadabu,

Aminadabu alizaa Kora,

Kora alizaa Asiri,

Asiri alizaa Elekana,

Elekana alizaa Ebiasafi,

Ebiasafi alizaa Asiri,

Asiri alizaa Tahati,

Tahati alizaa Urieli,

Urieli alizaa Usia,

Usia alizaa Saulo.

10-13Elekana alizaa Amasai na Ahimoti.

Ahimoti alizaa Elekana,

Elekana alizaa Zofai,

Zofai alizaa Nahati,

Nahati alizaa Eliabu,

Eliabu alizaa Yerohamu,

Yerohamu alizaa Elkana.

Wana wa Samweli walikuwa wawili: Yoeli, muzaliwa wake wa kwanza, na Abiya, mudogo wake.

14-15Uzao wa Merari:

Merari alizaa Mali,

Mali alizaa Libuni,

Libuni alizaa Simei,

Simei alizaa Uza,

Uza alizaa Simea,

Simea alizaa Hagia,

Hagia alizaa Asaya.

Waimbaji wa hekalu

16Hawa ndio watu ambao mufalme Daudi aliweka kwa kazi ya kuimba katika nyumba ya Yawe, nyuma ya kuwekwa kwa Sanduku la Agano ndani yake. Ang. Kut 6.16-19

17Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mukutano mpaka wakati mufalme Solomono alipojenga hekalu la Yawe kule Yerusalema. Walitumika kazi yao vizuri kufuatana na zamu ya kila kundi.

18-23Hizi ndizo ukoo za wale ambao walifanya kazi hizo:

Kutoka ukoo wa Kohati, kulikuwa Hemani, kiongozi wa kundi la kwanza la waimbaji. Hemani alikuwa mwana wa Yoeli, Yoeli wa Samweli, Samweli wa Elekana, Elekana wa Yerohamu, Yerohamu wa Elieli, Elieli wa Toa, Toa wa Zufi, Zufi wa Elekana, Elekana wa Mahati, Mahati wa Amasai, Amasai wa Elekana, Elekana wa Yoeli, Yoeli wa Azaria, Azaria wa Sefania, Sefania wa Tahati, Tahati wa Asiri, Asiri wa Ebiasafu, Ebiasafu wa Kora, Kora wa Izihari, Izihari wa Kohati, Kohati wa Lawi, Lawi wa Israeli.

24-28Asafu, ndugu ya Hemani alikuwa kwa upande wake wa kuume. Asafu alikuwa mwana wa Berekia, Berekia wa Simea, Simea wa Mikaeli, Mikaeli wa Basea, Basea wa Malkia, Malkia wa Etini, Etini wa Zera, Zera wa Adaya, Adaya wa Etani, Etani wa Zima, Zima wa Simei, Simei wa Yahati, Yahati wa Gersoni, Gersoni wa Lawi.

29-32Etani wa ukoo wa Merari, alikuwa kiongozi wa kundi la tatu la waimbaji. Etani alikuwa mwana wa Kisi, Kisi wa Abudi, Abudi wa Maluku, Maluku wa Hasabia, Hasabia wa Amazia, Amazia wa Hilkia, Hilkia wa Amusi, Amusi wa Bani, Bani wa Semeri, Semeri wa Mali, Mali wa Musi, Musi wa Merari, Merari wa Lawi.

33Ndugu zao wengine walipewa kazi zingine katika hema takatifu la nyumba ya Mungu.

Wazao wa Haruni

34Haruni na wazao wake ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya mazabahu ya sadaka za kuteketezwa kwa moto na vilevile juu ya mazabahu ya kufukizia ubani. Walifanya kazi zote zilizoelekea Pahali Patakatifu Sana kwa kuifanyia Israeli upatanisho. Haya yote waliyafanya kulingana na maagizo Musa, mutumishi wa Mungu aliyotoa.

35-38Hawa ndio wazao wa Haruni:

Haruni alizaa Eleazari,

Eleazari alizaa Finehasi,

Finehasi alizaa Abisua,

Abisua alizaa Buki,

Buki alizaa Usi,

Usi alizaa Serahia,

Serahia alizaa Merayoti,

Merayoti alizaa Amaria,

Amaria alizaa Ahitubu,

Ahitubu alizaa Zadoki,

Zadoki alizaa Ahimasi.

39Huu ndio urizi wao kulingana na mipaka yake: wazao wa Haruni katika jamaa ya Wakohati kulingana na kura yao,

40hao walipewa muji wa Hebroni katika inchi ya Yuda na mashamba ya malisho kandokando yake.

41Lakini mashamba katika muji pamoja na mashamba yake ya malisho yalitolewa kwa Kalebu mwana wa Yefune.

42Wazao wa Haruni wakapewa miji ya makimbilio: Hebroni, Libuna pamoja na mashamba yake ya malisho, Yatiri na Estemoa pamoja na mashamba yake ya malisho,

43Hileni na Debiri pamoja na mashamba yake ya malisho,

44Asani na Beti-Semesi pamoja na mashamba yake ya malisho.

45Katika eneo la kabila la Benjamina wakapewa miji ya Geba, Alemeti na Anatoti pamoja na malisho ya miji hiyo. Miji yote waliyopewa kulingana na jamaa zao ilikuwa kumi na mitatu.

46Miji kumi ya eneo la nusu ya kabila la Manase ilitolewa kwa sehemu iliyobaki ya ukoo wa Kohati kwa kura kulingana na jamaa zao.

47Ukoo wa Gersoni, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Nafutali na katika kabila la Manase katika Basani.

48Vilevile, miji kumi na miwili katika kabila la Rubeni, na katika kabila la Gadi na katika kabila la Zebuluni ilipewa ukoo wa Merari kulingana na jamaa zao.

49Kwa njia hii watu wa Israeli waliwapa Walawi miji kusudi waishi ndani yake pamoja na mashamba ya malisho ya miji hiyo.

50(Miji iliyotajwa majina hapa juu katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni na katika kabila la Benjamina iligawanyiwa kwa kabila la Lawi kwa kura.)

51Jamaa zingine za ukoo wa Kohati zilipewa miji pamoja na malisho yake katika kabila la Efuraimu:

52Sekemu, muji wa makimbilio katika inchi ya milima ya Efuraimu pamoja na mashamba yake ya malisho, Gezeri pamoja na malisho yake,

53Yokimeamu pamoja na mashamba yake ya malisho, Beti-Horoni pamoja na mashamba ya malisho yake;

54Ayaloni pamoja na mashamba yake ya malisho, na Gati-Rimoni pamoja na mashamba yake ya malisho.

55Katika nusu ya kabila la Manase walipewa miji ya Aneri pamoja na mashamba yake ya malisho, na Bileamu pamoja na mashamba yake ya malisho. Hii ndiyo miji iliyopewa kwa jamaa za ukoo wa Kohati.

56Jamaa za ukoo wa Gersoni walipewa miji hii pamoja na mashamba yake ya malisho: katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Basani pamoja na mashamba yake ya malisho, Astaroti pamoja na mashamba yake ya malisho.

57Katika kabila la Isakari walipewa: Kedesi pamoja na mashamba yake ya malisho, Deberati pamoja na mashamba yake ya malisho,

58Ramoti pamoja na mashamba yake ya malisho na Anemu pamoja na malisho yake.

59Katika kabila la Aseri walipewa: Masali pamoja na mashamba yake ya malisho, Abudoni pamoja na mashamba yake ya malisho,

60Hukoki pamoja na mashamba yake ya malisho, na Rehobu na malisho yake.

61Katika kabila la Nafutali: Kedesi katika Galilaya pamoja na mashamba yake ya malisho, Hamoni pamoja na mashamba yake ya malisho na Kiriataimu pamoja na mashamba yake ya malisho.

62Jamaa za Merari zilizobakia, zilipewa miji hii pamoja na mashamba yake ya malisho kandokando ya miji hiyo.

Katika kabila la Zebuluni walipewa Rimono pamoja na mashamba yake ya malisho na Tabori pamoja na mashamba yake ya malisho.

63Katika kabila Rubeni, upande wa mashariki ya muto Yordani karibu na muji wa Yeriko walipewa Bezeri unaokuwa katika inchi ya vilima pamoja na mashamba yake ya malisho, Yahasa pamoja na mashamba yake ya malisho,

64Kedemoti pamoja na mashamba yake ya malisho na Mefati pamoja na mashamba yake ya malisho.

65Katika kabila la Gadi walipewa Ramoti katika Gileadi pamoja na malisho yake, Mahanaimu pamoja na mashamba yake ya malisho,

66Hesiboni pamoja na mashamba yake ya malisho na Yazeri pamoja na mashamba yake ya malisho.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help