2 Wafalme UTANGULIZI - Swahili Congo Revised Bible 2002

UTANGULIZIKatika kitabu hiki tunapewa habari za utawala wa wafalme wa mwisho wa tawala za Yuda na Israeli. Sehemu ya kwanza ya kitabu hiki (sura 1-17) inaelekea habari za Ahazia mufalme wa Israeli mpaka wakati wa kuangamizwa kwa utawala wa kaskazini ni kusema Israeli, katika mwaka 722 mbele ya Kristo. Sura nyingi za sehemu hii zinatupatia habari za nabii Elisha ambaye alishika nafasi ya Elia (sura 2-13).Sehemu ya pili ya kitabu hiki (sura 18-25) inaelekea mambo ya miaka 130 ambayo yalitokea katika utawala wa kusini, ni kusema Yuda, mpaka wakati Nebukadneza mufalme wa Babeli, alipoushambulia muji wa Yerusalema katika mwaka 587 mbele ya Kristo, akaliharibu hekalu na kuwapeleka watu wengi wenye sifa wa Yuda mpaka Babeli (sura 25). Hasara hizo zilizoupata utawala wa Yuda na yale yaliyoupata utawala wa Israeli, yanaelezwa kuwa matokeo ya ukosefu wa imani kwa Mungu.
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help