1Mashairi ya Daudi.
Unilinde,
ee Mungu,
maana ninakimbilia kwako.
2Ninamwambia Mungu: “Wewe ni Bwana wangu;
sina uheri wowote isipokuwa wewe.”
3Na juu ya waaminifu katika inchi,
ninaheshimu nguvu zao.
4Lakini wanaoabudu miungu mingine,
watapata mateso mengi.
Sitaitolea sadaka za damu hata kidogo,
na majina ya miungu hiyo sitayataja.
5Wewe, ee Yawe, ndiwe riziki yangu kubwa,
majaliwa yangu yako katika mikono yako.
6Umenipimia sehemu nzuri sana;
urizi wangu ni wa kupendeza.
7Ninamusifu Yawe anayeniongoza.
Usiku zamiri yangu inanifundisha.
8Siku zote Yawe ni mbele yangu;
yeye yuko pamoja nami, wala sitatikisika.
9Kwa hiyo nitafurahi kwa moyo wote na kushangilia,
nami nitakaa salama kabisa.
10Kweli wewe unanikinga na nguvu za kuzimu,
haumwachi mutakatifu wako aone kaburi.
11Unanionyesha njia ya kufikia uzima.
Kuwa mbele yako ni kujazwa furaha,
kuwa kwa kuume kwako kunapendeza milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.