Yobu 39 - Swahili Congo Revised Bible 2002

1Unajua mbuzi wa milima anazaa wakati gani,

au umekwisha kuona kulungu akizaa?

2Unajua anapata mimba kwa muda gani,

au siku yenyewe ya kuzaa unaijua?

3Wanachutama kwa kuzaa,

wanazaa vitoto vyao.

4Vitoto vyao vinapata nguvu,

vinakomaa kulekule katika pori,

kisha vinawaacha wamama zao na kwenda zao.

5Nani aliyemwacha huru punda wa pori?

Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua?

6Mimi niliwapa jangwa likuwe nyumba yao,

mbuga zenye chumvi kuwa makao yao.

7Wanajitenga kabisa na makelele ya miji,

hawasikilizi kelele la muchungaji.

8Wanatembeatembea katika milima kwa kupata malisho,

na kutafuta kitu chochote kinachokuwa kibichi.

9Mbogo atakubali kukutumikia?

Atakubali kulala katika zizi lako?

10Unaweza kumufunga mbogo kamba kwa kulima shamba,

au akokote jembe la kulima?

11Utamutegemea kwa sababu ana nguvu nyingi

na kumwacha akufanyie kazi zako nzito?

12Unamutazamia mbogo akuvunie mavuno yako,

na kuleta ngano kwenye nafasi ya kupepetea?

13Mbuni anapigapiga mabawa yake kwa furaha,

lakini hawezi kuruka kama korongo.

14Mbuni anayaacha mayai yake juu ya udongo

kusudi yapate joto ndani ya muchanga;

15lakini hajui kama yanaweza kukanyagwa,

au kuvunjwa na nyama wa pori.

16Mbuni anatendea vitoto vyake kwa ukali kama vile si vyake,

hata kazi yake ikiharibika yeye hana wasiwasi;

17kwa sababu nilimufanya asahau hekima yake,

wala sikumupa sehemu yoyote ya akili.

18Lakini akianza kukimbia,

anamuchekelea hata farasi na mupanda-farasi.

19Yobu, ni wewe ndiwe uliyewapa farasi nguvu,

ukawavalisha kwenye shingo manyoya marefu?

20Ni wewe unayemufanya farasi aruke kama nzige?

Mulio wake wa maringo ni wa ajabu!

21Anakwaruzakwaruza udongo katika mabonde kwa pupa;

anakimbilia kwenye mapigano kwa nguvu zake zote.

22Farasi anaichekelea hofu, na hatishiki;

wala upanga hauwezi kumurudisha nyuma.

23Silaha wapanda-farasi wanazobeba,

zinagongana kwa sauti na kuangaa kwenye jua.

24Farasi anasonga mbele, akitetemeka kwa hasira;

baragumu inapolia, yeye hasimami.

25Kila mara baragumu inapopigwa, yeye anatoa sauti;

anasikia harufu ya vita toka mbali,

anasikia mushindo wa majemadari

wakitoa amri kwa makelele.

26Mwewe amejifunza kwako jinsi ya kuruka,

na kunyoosha mabawa yake kuelekea upande wa kusini?

27Tai anapanda juu kwa amri yako,

na kuweka chicha yake juu kwenye milima?

28Tai anafanya makao yake juu ya mawe marefu,

na incha kali za mawe makubwa ndizo maficho yake.

29Kutoka kule anavizia nyama,

macho yake yanaiona kutoka mbali.

30Vitoto vyake vinafyonza damu;

pale muzoga unapokuwa ndipo tai anapokuwa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help