Yoshua 19 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Inchi kabila la Simeoni waliyopewa

1Kura ya pili ilizipata ukoo za kabila la Simeoni na sehemu yao ya inchi ilikuwa imezungukwa na ile ya kabila la Yuda.

2-8Kabila la Simeoni lilipata miji ya:

Beri-Seba, Seba, Molada,

Hasari-Suali, Bala, Ezemu,

Eltoladi, Betuli, Horma,

Ziklagi, Beti-Makaboti, Hasari-Susa,

Beti-Lebaoti na Saruheni.

Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.

Vilevile kulikuwa miji ya Aini, Rimoni, Eteri, na Asani.

Jumla ya miji mine pamoja na vijiji vyake, pamoja na vijiji vyote vilivyoizunguka miji hiyo mpaka Balati-Beri na Rama ya Negebu.

Hiyo yote ni sehemu zilizopewa ukoo za kabila la Simeoni. Ang. 1 Sik 4.28-33

9Kwa vile eneo lililopewa kabila la Yuda lilikuwa kubwa kuliko kabila hilo lilivyohitaji, sehemu ya eneo lake lilipewa kabila la Simeoni.

Inchi kabila la Zebuluni waliyopewa

10Kura ya tatu ilizipata ukoo za kabila la Zebuluni. Eneo lao lilienea mpaka Saridi.

11Kutokea kule mupaka wake ulikwenda upande wa magaribi hata Marali, ukapitia pembeni ya Dabeseti na kwenda kwenye kijito kinachokuwa upande wa mashariki wa Yokinamu.

12Kutokea Saridi, mupaka ule ulielekea mashariki hata kwenye mupaka wa Kisiloti-Tabori, na kutokea kule ukapita Daberati mpaka Yafia.

13Kutokea Yafia uliendelea upande wa mashariki hata Gati-Heferi, Eti-Kasini, na kuendelea mpaka Rimoni ambako ulipanda kuelekea Nea.

14Upande wa kaskazini mupaka uligeuka kuelekea Hanatoni na kuishia kwenye bonde la Ifitaheli.

15Ukakusanya miji ya Katati, Nahalali, Simuroni, Idala na Betelehemu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.

16Hiyo ndiyo sehemu zilizopewa ukoo za kabila la Zebuluni miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Inchi ya kabila la Isakari

17Kura ya ine ilizipata ukoo za kabila la Isakari.

18-22Eneo lenyewe lilikuwa na miji ya:

Yezereheli, Kesuloti, Sunemu,

Hafaraimu, Sioni, Anaharati,

Rabiti, Kisioni, Ebesi,

Remeti, Eni-Ganimu, Eni-Hada na Beti-Pasesi.

Vilevile, mupaka wao ulifika Tabori, Sahasuma, Beti-Semesi na kuishia kwenye muto Yordani.

Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na sita pamoja na vijiji vyake.

23Hiyo ndiyo sehemu zilizopewa ukoo za kabila la Isakari; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Inchi ya kabila la Aseri

24Kura ya tano ilizipata ukoo za kabila la Aseri.

25Eneo la inchi yao lilikuwa na miji ya: Helkati, Hali, Beteni, Akisafu,

26Alameleki, Amadi na Misali. Kwa upande wa magaribi mupaka uligusana na Karmeli na Sihori-Libunati.

27Kisha ukageuka kuelekea mashariki kwenda Beti-Dagoni ambako unagusana na Zebuluni na bonde la Ifitaheli. Halafu ukaendelea kaskazini ukafika Beti-Emeki, Neieli na kuzidi kuelekea kaskazini ukafika Kabuli,

28Eburoni, Rehobu, Hamoni, Kana mpaka Sidona muji mukubwa.

29Hapo, mupaka uligeuka kuelekea Rama na kufikia kwenye muji wa Tiro uliokuwa na kuta. Kisha ukageuka kuelekea Hosa na kuishia kwenye bahari ya Mediteranea. Miji mingine iliyokuwa katika eneo lile ni Maharabu, Akizibu,

30Uma, Afeki na Rehobu. Jumla ya miji waliyopewa ni makumi mbili na mbili pamoja na vijiji vyake.

31Hiyo ndiyo sehemu zilizopewa ukoo za kabila la Aseri; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Inchi ya kabila la Nafutali

32Kura ya sita ilizipata ukoo za kabila la Nafutali.

33Mupaka wake ulianzia Helefi na kwenye muti wa mwalo wa Zananimu, ukapita Adami-Nekebu na Yabuneli ukafika Lakumu na kuishia kwenye muto Yordani.

34Kutoka pale mupaka ulikwenda upande wa magaribi kuelekea Asinoti-Tabori; tokea kule ukaenda Hukoki na kugusana na pembe ya kusini ya eneo la kabila la Zebuluni; kisha kugusana na eneo la kabila la Aseri upande wa magaribi, na kugusana na eneo la kabila la Yuda. Kwa upande wa mashariki mupaka uliingilia kwenye muto Yordani.

35-38Miji yao iliyokuwa na kuta ni:

Zidimu, Zeri, Hamati, Rakati, Kinereti,

Adama, Rama, Hazori,

Kedesi, Edirei, Eni-Hazori,

Ironi, Migdali-Eli, Horemu,

Beti-Anati na Beti-Semesi.

Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na tisa pamoja na vijiji vyake.

39Hiyo ndiyo sehemu zilizopewa ukoo za kabila la Nafutali; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Inchi ya kabila la Dani

40Kura ya saba ilizipata ukoo za kabila la Dani.

41-46Eneo la inchi yao lilikuwa na miji ya:

Zora, Estaoli, Iri-Semesi,

Salabinu, Ayaloni, Itila,

Eloni, Timuna, Ekuroni,

Elteke, Gibetoni, Balati,

Yehudi, Bene-Beraki, Gati-Rimoni,

Me-Yarkoni na Rakoni na inchi iliyokuwa karibu na Yopa.

47Watu wa kabila la Dani walipopoteza inchi yao, walikwenda na kuushambulia muji wa Lesemu. Waliushinda na kuuteka, na nyuma ya kuwaua wakaaji wake wote, wakaurizi halafu wakabadilisha jina la muji ule kuwa Dani; jina ambalo lilikuwa ni la babu yao. Ang. Amu 18.27-29

48Hiyo ndiyo sehemu zilizopewa ukoo za kabila la Dani; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Ugawanyaji wa mwisho

49Walipomaliza kugawanyana sehemu zote za inchi, Waisraeli walimupa Yoshua mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao.

50Kulingana na amri ya Yawe walimupa muji ambao aliuchagua yeye mwenyewe, ni kusema Timunati-Sera, ambao ulikuwa katika inchi ya milima ya Efuraimu. Naye Yoshua akaujenga upya muji ule na kukaa mule.

51Basi, kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawanya sehemu hizo kwa kura mbele ya Yawe kwenye mulango wa hema ya kusanyiko kule Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawanya inchi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help