1Halafu Yobu akajibu:
2Mambo kama yale nimeyasikia mengi;
ninyi ni wafariji wenye kutaabisha!
3Mwisho wa maneno haya ya bure ni wakati gani?
Au ni kitu gani kinachowasukuma kujibu?
4Kama mungekuwa mimi, na mimi ninyi,
ningeweza kusema kama ninyi.
Ningeweza kutunga maneno juu yenu,
na kutikisa kichwa changu.
5Ningeweza kuwatia moyo kwa maneno yangu,
na maneno yangu ya faraja yangewatuliza.
6Lakini nikisema maumivu yangu hayatulii,
na nikikaa kimya hayaondoki.
7Kweli Mungu amenichakalisha,
ameharibu kila kitu karibu nami.
8Amenifanya ninyauke na huo ni ushuhuda juu yangu.
Kukonda kwangu kumenishitaki
na kushuhudia juu yangu.
9Amenirarua kwa hasira na kunichukia,
amenisagia meno,
na adui yangu ananitonolea macho.
10Watu wanafungua vinywa vyao na kunichekelea.
Makundi kwa makundi wananizunguka
na kunipiga makofi kwenye mashavu.
11Mungu amenitia katika mikono ya wapotovu
na kunitupa katika mikono ya waovu.
12Nilikuwa nimestarehe, lakini akanivunjavunja.
Alinikamatia katika shingo na kunipasua vipandevipande.
Akanifanya shabaha ya mishale yake,
13akanipiga mishale kutoka kila upande.
Amenipasua figo bila huruma,
na nyongo yangu akaimwanga chini.
14Ananivunja na kunipiga tena na tena;
ananishambulia kama askari.
15Nimejishonea nguo za gunia;
utukufu wangu nikautupa katika mavumbi.
16Macho yangu ni mekundu kwa sababu ya kulia,
kope zangu zimekuwa nyeusi sana,
17ingawa sijatesa watu kwa mukono wangu,
na maombi yangu kwa Mungu ni safi.
18Ewe dunia, usifunike damu yangu iliyomwangika;
kilio changu kienee kila pahali.
19Nina uhakika kwamba nina mushuhuda wangu mbinguni;
mwenye kunitetea yuko kule juu.
20Warafiki zangu wanizarau;
ninatoa machozi kumwomba Mungu.
21Heri mutu angenitetea mbele ya Mungu,
kama vile inavyofanyika katika dunia kati ya watu wawili.
22Kweli, miaka yangu ni michache,
nami nitakwenda kule ambako sitarudi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.