Zaburi 133 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Uzuri wa umoja kati ya watu

1Wimbo wa safari za kidini: wa Daudi.

Ni jambo zuri na la kupendeza sana kwa

ndugu kuishi pamoja kwa umoja.

2Ni kama mafuta mazuri yanayotiririka juu ya kichwa,

mpaka kwenye ndevu za Haruni,

mpaka juu ya upindo wa nguo yake kwenye shingo.

3Ni kama umande wa mulima Hermoni,

unaoanguka juu ya vilima vya Sayuni!

Kutoka huko Yawe anatoa baraka,

ndio uzima wa milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help