1Wimbo wa safari za kidini.
Ninainua macho kwenye milima.
Musaada wangu unatoka wapi?
2Musaada wangu unatoka kwa Yawe,
aliyeumba mbingu na dunia.
3Hatakuacha uanguke;
mulinzi wako hasinzii.
4Kweli mulinzi wa Israeli
hasinzii wala halali.
5Yawe ni mulinzi wako;
yuko upande wako wa kuume kwa kukukinga.
6Muchana jua halitakuchoma,
wala mwezi hautakuzuru usiku.
7Yawe atakukinga na uovu wote;
atayalinda salama maisha yako.
8Yawe atakulinda katika shuguli zako zote
tangu sasa na hata milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.