1Kwa siku ya tano ya mwezi wa ine, mwaka wa makumi tatu, wakati nilipokuwa katikati ya wale watu waliopelekwa katika uhamisho, karibu na muto Kebari, mbingu zikafunguka, nikapata maono toka kwa Mungu.
2Katika siku ya tano ya mwezi (ulikuwa mwaka wa tano tangu mufalme Yoyakinu alipopelekwa katika uhamisho katika Babeli), kila kimoja kilikwenda mbele moja kwa moja pasipo kugeuka.
13Katikati ya vile viumbe kulikuwa kitu kilichoonekana kama mienge ya moto iliyoangaza huku na huku kati ya hivyo viumbe. Moto huo ulikuwa ukiwaka sana na umeme ulitokea humo.
14Viumbe vile vilikwenda na kurudia mbio kama vile umeme unavyoonekana.
15Nilipokuwa nikiangalia viumbe vile, nikaona chini karibu na kila kiumbe kulikuwa gurudumu. Ang. Eze 10.9-13
16Magurudumu hayo yalionekana kuwa ya namna moja, yanametameta kama jiwe la zabarajadi na umbo lao lilikuwa kama gurudumu ndani ya gurudumu lingine.
17Yalipotembea yalikwenda kwa pande zote ine pasipo kugeuka yanapokwenda.
18Miviringo ya hayo magurudumu ilikuwa mirefu na ya kuogopesha nayo ilikuwa inajaa macho pande zote. Ang. Ufu 4.8
19Vile viumbe vilipokwenda, magurudumu nayo yalikwenda kandokando yao; na viumbe vile viliponyanyuka juu kutoka kwenye udongo, magurudumu hayo yaliinuka.
20Popote roho alipokwenda vilikwenda, nayo magurudumu yaliinuka pamoja navyo; maana roho ya hivyo viumbe ilikuwa katika magurudumu hayo.
21Viumbe hivyo vilipokwenda, magurudumu nayo yalikwenda; viliposimama, nayo yalisimama; vilipoinuka juu kutoka kwenye udongo, magurudumu nayo yaliinuka pamoja navyo. Maana roho wa vile viumbe vya ajabu ilikuwa katika magurudumu hayo.
22Juu ya vichwa vya vile viumbe kulikuwa kitu kinachofanana na anga, kinangaa kama kioo. Ang. Ufu 4.6
23Viumbe vile vilisimama chini ya kitu hicho; mabawa mawili ya vile viumbe yalikuwa yamekunjuliwa, moja likielekea lingine, na kwa mabawa mengine mawili vilifunika miili yao.
24Vilipokuwa vinakwenda, nilisikia sauti ya mabawa yao; sauti ya muvumo huo ilikuwa kama ile ya maji mengi, kama sauti ya ngurumo kutoka kwa Mungu wa majeshi, na kama kelele ya jeshi. Viliposimama, vilikunja mabawa yao.
25Nilisikia sauti kutoka juu ya kitu kile kinachokuwa kama anga kilichokuwa juu ya vichwa vyao.
26Juu ya kitu hicho niliona kitu kimoja kinachofanana na kiti cha kifalme chenye rangi la jiwe la yakuti. Juu yake kulikuwa kunaikaa kitu kinachofanana na mutu. Ang. Eze 10.1; Ufu 4.2-3
27Sehemu ya juu ya mwili wake ilingaa kama shaba, nao ulikuwa sawa unazungukwa na moto pande zote. Tokea sehemu ya chini ya mwili wake, niliona kitu kama moto. Mwangaza ulimuzunguka. Ang. Eze 8.2
28Ulionekana kama upindi wa mvua wakati wa mvua. Ulionekana kufanana na utukufu wa Yawe. Nilipouona, nilianguka uso mpaka chini, nikasikia sauti ya mutu mwenye kusema.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.