1Naye akaniambia: Wewe mwanadamu! Simama. Ninataka kusema nawe.
2Alipokuwa akisema nami, Roho wa Mungu akaniingia na kunisimamisha wima. Halafu nikamusikia
3akiniambia hivi: Wewe mwanadamu ninakutuma kwa Waisraeli, taifa la waasi ambao wameniasi. Wameendelea kunikosea mimi mpaka leo sawa vile babu zao walivyofanya.
4Watu hao ni wenye kichwa nguvu na moyo mugumu. Ninakutuma kwao, nawe utawaambia: “Bwana wetu Yawe anasema hivi.”
5Wakisikia au wakikataa kusikia, maana hao ni watu waasi, watatambua kwamba nabii yuko katikati yao.
6Lakini, ewe mwanadamu usiwaogope hao wala maneno yao; maana uko katikati ya michongoma na miiba, nawe unaikaa pamoja na nge; usiogope maneno yao wala usitishwe na nyuso zao, maana hao ni watu waasi.
7Wewe utawaambia maneno yangu, wakisikia au wakikataa kusikia, maana hao ni watu waasi.
8Lakini, ewe mwanadamu, usikilize ninayokuambia, wala usikuwe mwasi kama watu hao waasi. Ufungue kinywa chako, ukule ninachokupa.
9Nilipoangalia, nikaona nimenyooshewa mukono, nao ulikuwa ukishika kitabu kilichozingwa. Ang. Ufu 5.1
10Basi akakikunjua mbele yangu, nacho kilikuwa kimeandikwa mbele na nyuma maneno ya maombolezo, kilio na hasara.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.