Zaburi 51 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Kuomba usamehe

1-2Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi inayoelekea wakati nabii Natani alipomufikia kwa kumwonya juu ya uzinzi alioufanya na Batiseba.

3Unihurumie, ee Mungu,

kadiri ya wema wako;

uyafute makosa yangu,

kadiri ya wingi wa rehema yako.

4Unisafishe kabisa kosa langu;

unitakase zambi yangu.

5Ninaitikia kabisa makosa yangu,

siku zote ninaona waziwazi zambi yangu.

6Nimekukosea wewe peke yako,

nimetenda mabaya mbele yako.

Hivi uamuzi wako ni wa haki,

hukumu yako haipotoki.

7Mimi ni mukosaji tangia kuzaliwa kwangu,

mwenye zambi tangia tumbo la mama yangu.

8Wewe unataka moyo wa ukweli;

hivyo unifundishe kuwa na moyo wa hekima.

9Unitakase kwa hisopo, nikuwe safi,

unisafishe, nikuwe mweupe pee.

10Unijaze furaha na shangwe,

unifurahishe tena, mimi ambaye uliniponda.

11Ugeuke, usiangalie zambi zangu;

uyafute makosa yangu yote.

12Ee Mungu, uniumbie moyo safi,

uweke ndani yangu roho mupya na inayoimarika.

13Usinitupe mbali nawe;

usiondoe roho yako takatifu ndani yangu.

14Unirudishie furaha ya wokovu wako,

uniimarishe kwa Roho wako mwema.

15Halafu nitawafundisha wakosaji njia zako,

nao wenye zambi watarudi kwako.

16Uniokoe kutoka kosa la kumwanga damu,

ee Mungu, Mungu mwokozi wangu,

nami nitaimba kwa sauti kwamba umeniokoa.

17Ee Bwana, uniwezeshe kusema,

midomo yangu itangaze sifa zako.

18Kweli wewe haupendezwi na sadaka.

Hautaki nikutolee sadaka za kuteketezwa.

19Sadaka ninayokutolea, ee Mungu, ni roho munyenyekevu.

Haukatai moyo munyenyekevu na wa kutubu.

20Ee Mungu, upendezwe na kuutendea mazuri Sayuni;

uzijenge tena upya kuta za Yerusalema.

21Halafu utapendezwa na sadaka za haki:

ndizo sadaka za kuteketezwa na za kuteketezwa nzima.

Ngombe dume watatolewa juu ya mazabahu yako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help