Yobu 24 - Swahili Congo Revised Bible 2002

1Mbona Mungu Mwenye Uwezo hapangi wakati wa hukumu?

Kwa nini wanaomujua hawajui hizo siku zake?

2Watu wanaondoa vitambulisho vya mipaka ya mashamba,

na wengine wanaiba makundi ya nyama na kuwafuga.

3Wananyanganya wayatima punda wao,

wanatwaa ngombe dume wa mujane kuwa rehani.

4Wanasukuma wamasikini kandokando ya barabara;

wamasikini wa dunia wanajificha mbele yao.

5Kwa hiyo kama punda wa pori katika jangwa,

wanatoka mapema kwenda kutumika,

wakitafuta chakula kwa bidii,

kusudi wapate chochote cha kukulisha watoto wao.

6Wamasikini wanalazimishwa kuvuna mashamba ya wengine,

wanaokota katika shamba la mizabibu la waovu.

7Usiku kucha wanalala uchi bila nguo,

wakati wa baridi hawana cha kujifunikia.

8Wanalowana kwa mvua ya juu ya milima,

wanajibanisha kwenye mawe kwa ukosefu wa makimbilio.

9Kuna watu wanaoondoa watoto wayatima kwenye vifua vya mama yao.

Wengine wanatwaa nguo ya masikini kuwa rehani.

10Wamasikini wanatembea uchi, bila nguo;

wenye njaa wanabeba miganda ya ngano.

11Wanawatengenezea waovu mafuta yao,

au kukamua divai bila hata kuionja.

12Kutoka katika muji, kilio cha wanaokufa kinasikilika,

na walioumizwa wanalalamika kuomba musaada.

Lakini Mungu hasikilizi kabisa maombi yao.

13Kuna wengine waovu wasiopenda mwangaza,

wasiofahamu njia za mwangaza,

na hawapendi kushika njia zake.

14Mwuaji anaamuka asubui mapema,

kwa kwenda kuwaua wamasikini na wakosefu,

na usiku ukifika, kazi yake ni kuiba.

15Muzinzi naye anangojea giza liingie,

akisema: “Hakuna atakayeniona”;

kisha anaficha uso wake kwa nguo.

16Usiku wezi wanavunja nyumba,

lakini muchana wanajifungia ndani;

wala hawajui kabisa mwangaza ni nini.

17Kwao wote giza kubwa ni mwangaza wa asubui;

wao ni warafiki za vitisho vya giza kubwa.

18Lakini munasema: “Waovu wanapelekwa haraka na mafuriko ya maji,

makao yao yanabaki kuwa inchi iliyolaaniwa;

hakuna anayeenda kwenye mashamba yao ya mizabibu.”

19Kama vile teluji inavyoyeyuka katika joto na kipwa

ndivyo kuzimu inavyotowesha waovu.

20Maana muzazi wao anawasahau watu hao,

hakuna atakayewakumbuka tena.

Ndivyo uovu ulivyovunjika kama muti.

21Waovu wanatesa wanawake wasiopata watoto

wala hawawatendei vizuri wanawake wajane.

22Mungu, kwa nguvu yake, anawaangamiza wenye uwezo;

anasimama, nao wanakata tamaa ya kuishi.

23Anawaacha waovu wajione salama,

lakini macho yake yanachunguza mienendo yao.

24Waovu wanafanikiwa kwa muda tu, kisha wanatoweka,

wananyauka na kufifia kama vile jani,

wanakatwa kama vile masuke ya ngano.

25Nani basi, anayeweza kuhakikisha kwamba mimi ni mwongo

na kuonyesha kwamba maneno yangu si kweli?

Jibu la Bildadi
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help