Yeremia 45 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Ahadi ya Mungu kwa Baruku

1Haya ndiyo maneno nabii Yeremia aliyosema katika mwaka wa ine wa utawala wa Yoyakimu mwana wa Yosia, mufalme wa Yuda na Baruku mwana wa Neria akayaandika katika kitabu:

2Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi juu yako wewe Baruku:

3Wewe ulisema: Ole wangu! Yawe ameongezea uchungu juu ya maumivu yangu. Nimechoka na kulalamika, wala siwezi kupumzika.

4Lakini Yawe ameniambia nikuambie:

Yawe anasema hivi: Yale niliyojenga ninayabomoa, na yale niliyopanda ninayaongoa; nitafanya hivyo katika inchi yote.

5Wewe unajitakia wewe mwenyewe mambo makubwamakubwa? Usiyatafute! Achana nayo, maana ninaleta maangamizi juu ya wanadamu wote. Pato lako ni hili: nitayaokoa maisha yako kila nafasi utakapokwenda.

–Ni ujumbe wa Yawe.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help