1Ingeteketea kama moto unavyochoma kichaka,
kama vile moto unavyochemusha maji.
Ukuje upate kuwajulisha waadui zako jina lako
nayo mataifa yatetemeke mbele yako!
2Wakati ulipotenda maajabu ambayo hatukutazamia,
ulishuka chini nayo milima ikatetemeka ilipokuona.
3Tangu zamani hakuna aliyepata
kusikia kwa masikio yake wala kumwona
Mungu anayekuwa kama wewe,
anayetenda mambo kama hayo kwa ajili ya wale wanaomutegemea!
4Wewe unakuja kuwasaidia wanaotenda haki kwa furaha,
wanaokukumbuka na kufuata njia zako.
Ulitukasirikia tulipokuwa wenye zambi;
sisi tumeasi kwa muda murefu.
5Sisi wote tumekuwa kama watu wachafu;
matendo yetu yote mema ni kama nguo chafu.
Wote tunanyauka kama majani,
uovu wetu unatupeperusha kama upepo.
6Hakuna hata mumoja anayekuja kukuomba;
hakuna anayejishugulisha kukutafuta.
Wewe unauficha uso wako mbali nasi,
umetuacha tufungwe na maovu yetu.
7Hata hivyo, ee Yawe, wewe ni Baba yetu.
Sisi ni kama udongo, wewe ni mufinyanzi.
Sisi wote ni kazi ya mikono yako.
8Usitukasirikie sana, ee Yawe,
usiukumbuke uovu wetu siku zote!
Ukumbuke kwamba sisi wote ni watu wako!
9Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa;
Sayuni umekuwa matongo,
Yerusalema umekuwa uharibifu.
10Nyumba yetu takatifu na nzuri,
ambamo babu zetu walikusifu,
imeteketezwa kwa moto.
Pahali petu pote pazuri pamekuwa mabomoko.
11Mbele ya hayo yote utajizuiza usifanye kitu?
Utaendelea kunyamaza tu, ee Yawe,
na kututesa kupita kipimo?
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.