Esteri UTANGULIZI - Swahili Congo Revised Bible 2002
UTANGULIZIKitabu cha Esteri kinasimulia jinsi Wayuda walivyookolewa kutoka vitisho vya kuangamizwa. Mambo hayo yalitokea kule katika muji wa Susani wakati utawala wa Persia ulipokuwa umeenea katika Mashariki ya Kati yote mpaka Misri. Wamoja kati ya jamaa zenye heshima za watu wa Israeli hawakurudia kwao kutoka Babeli wakati wa kuangamia kwa utawala wa Babeli (mwaka wa 539 mbele ya Kristo).