1Mashairi yanayoelekea muzinduo wa hekalu. Zaburi ya Daudi.
2Ninakutukuza,
ee Yawe,
maana umeniokoa,
wala haukuwaacha waadui zangu wanisimange.
3Ee Yawe, Mungu wangu,
nilikulilia, nawe ukaniponyesha.
4Ee Yawe, umeniokoa kutoka kuzimu;
umenipa tena uzima,
umenitoa kutoka kati ya wafu.
5Mumwimbie Yawe sifa, enyi waaminifu wake;
mukumbuke utakatifu wake na kumushukuru.
6Hasira yake inadumu muda kidogo tu,
upendo wake unadumu milele.
Kilio kinaweza kuwa usiku,
lakini muchana kunatokea furaha.
7Mimi nilipofanikiwa, nilisema:
“Sitashindwa hata kidogo!
8Kwa upendo wako, ee Yawe,
umeniimarisha kama mulima mukubwa.”
Lakini ukajificha mbali nami,
nami nikafazaika.
9Nilikulilia wewe, ee Yawe;
nilikusihi, ee Yawe:
10“Utapata faida gani nikikufa
na kushuka mpaka katika shimo la wafu?
Mavumbi ya wafu yanaweza kukusifu?
Yanaweza kusimulia uaminifu wako?
11Usikie, ee Yawe, unihurumie;
ee Yawe, unisaidie!”
12Wewe umegeuza malalamiko yangu kuwa ngoma ya furaha;
umeniondolea huzuni yangu, ukanijaza furaha.
13Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya.
Ee Yawe, Mungu wangu, nitakushukuru milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.