1-7Haya ndiyo majina ya makuhani na Walawi waliorudi toka katika uhamisho pamoja na Zerubabeli mwana wa Saltieli, na Kuhani Mukubwa Yesua.
Makuhani walikuwa:
Seraya, Yeremia, Ezra,
Amaria, Maluku, Hatusi,
Sekania, Rehumu, Meremoti,
Ido, Ginetoni, Abiya,
Miyamini, Madia, Bilga,
Semaya, Yoyaribu, Yedaya,
Salu, Amoki, Hilkia na Yedaya.
Hao walikuwa ni wakubwa wa makuhani na wandugu zao wakati wa Yesua.
8Walawi walikuwa:
Yesua, Binui, Kadimieli, Serebia, Yuda na Matania, ambaye alishugulika na usimamizi wa nyimbo za shukrani akishirikiana na ndugu zake.
9Nao Bakubukia na Uno warafiki zao, walisimama wakielekeana nao katika ibada.
Wazao wa Kuhani Mukubwa Yesua10-11Yesua alizaa Yoyakimu,
Yoyakimu alizaa Eliasibu,
Eliasibu alizaa Yoyada,
Yoyada alizaa Yonatani,
Yonatani alizaa Yadua.
Wakubwa wa ukoo za makuhani12-21Yoyakimu alipokuwa Kuhani Mukubwa, makuhani hawa walikuwa wakubwa wa ukoo zao:
ukoo wa Seraya: Meraya;
ukoo wa Yeremia: Hanania;
ukoo wa Ezra: Mehulamu;
ukoo wa Amaria: Yehohanani;
ukoo wa Maluku: Yonatani;
ukoo wa Sebania: Yosefu;
ukoo wa Harimu: Adina;
ukoo wa Meraioti: Helkayi;
ukoo wa Ido: Zakaria;
ukoo wa Ginetoni: Mesulamu;
ukoo wa Abiya: Zikiri;
ukoo wa Miniamini:
ukoo wa Moadia: Piltai;
ukoo wa Bilga: Samua;
ukoo wa Semaya: Yehonatani;
ukoo wa Yoaribu: Matenayi;
ukoo wa Yedaya: Uzi;
ukoo wa Salayi: Kalayi;
ukoo wa Amoki: Eberi;
ukoo wa Hilkia: Hesabia;
ukoo wa Yedaya: Netaneli.
Jamaa za makuhani na Walawi22Wakati wa Eliasibu, Yoyada, Yohanani na Yadua wakubwa wa jamaa za Walawi waliandikwa; vilevile wakati wa utawala wa mufalme Dario wakubwa wa jamaa za makuhani waliandikwa.
23Wakubwa wa jamaa za ukoo wa Lawi walioandikwa katika kitabu cha Mambo ya Siku mpaka wakati wa Yohanani mujukuu wa Eliasibu.
Utaratibu wa kazi katika hekalu24Viongozi wa Walawi Hasabia, Serebia, Yesua mwana wa Kadimieli walisimama kuelekeana na wandugu zao walipangwa kwa kuimba nyimbo za kusifu na kushukuru, kufuatana na amri ya mufalme Daudi, mutu wa Mungu.
25Walinzi wa milango walikuwa: Matania, Bakubukia, Obadia, Mesulamu, Talmoni na Akubu; vilevile hao walikuwa walinzi wa gala.
26Watu hao waliishi wakati wa Yoyakimu mwana wa Yesua mujukuu wa Yosadaki na vilevile wakati wa Nehemia aliyekuwa liwali wa jimbo; na hata wakati wa Ezra kuhani na mwandishi.
Nehemia anazindua ukuta27Kisha wakati wa kuzindua ukuta wa Yerusalema Walawi wakatafutwa kila pahali walipokaa kwa kuja Yerusalema kusherehekea kwa furaha pamoja na shukrani na nyimbo, wakitumia matoazi, vinubi na zeze.
28Wazao wa waimbaji wakakusanyika kutoka vijiji vya Yerusalema na vijiji vya Wanetofati,
29vilevile kutoka Beti-Gilgali, eneo la Geba na Azimaweti, kwa sababu waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kandokando ya Yerusalema.
30Makuhani na Walawi wakajitakasa, vilevile wakatakasa watu, milango na ukuta.
31Nikawakusanya viongozi wote wa Yuda kwenye ukuta na kutenga waimbaji katika makundi mawili makubwa yaliyoimba nyimbo za shukrani wakiwa katika maandamano. Kundi moja lilielekea upande wa kuume wa ukuta mpaka kwenye Mulango wa Takataka.
32Waimbaji hao walifuatwa na Hosaya akiwa pamoja na nusu ya viongozi wa Yuda.
33Pamoja naye walikwenda Azaria, Ezra, Mesulamu,
34Yuda, Benjamina, Semaya na Yeremia.
35Wazao hawa wa makuhani walikuwa na baragumu: Zakaria, mwana wa Yonatani mujukuu wa Semaya aliyekuwa mwana wa Matania mwana wa Mikaya mwana wa Zakuri mwana wa Asafu.
36Ndugu zake hawa waliimba kwa ala za muziki za mufalme Daudi, mutu wa Mungu, ni kusema Semaya, Azareli, Milalayi, Gilalayi, Maayi, Netaneli, Yuda na Hanani, wakatanguliwa na Ezra mwandishi.
37Kwenye Mulango wa Chemichemi walipanda ngazi kuelekea muji wa Daudi, wakapita nyumba ya kifalme ya Daudi, na kuelekea nyuma kwenye ukuta mpaka kwenye Mulango wa Maji, upande wa mashariki wa muji.
38Kundi lingine lililoimba nyimbo za shukrani lilielekea upande wa kushoto juu ya ukuta. Mimi nikafuatana na kundi hili pamoja na nusu ya watu. Tukapitia kwenye Munara wa Furu mpaka kwenye Ukuta Mupana.
39Na kutoka pale, tukapitia kwenye Mulango wa Efuraimu, Mulango wa Yesana, Mulango wa Samaki, Munara wa Hananeli, Munara wa Mia moja mpaka kwenye Mulango wa Kondoo. Tulimalizia maandamano yetu kwenye Mulango wa Walinzi.
40Hivyo, makundi yote mawili yaliyokuwa yanaimba nyimbo za shukrani yakasimama katika nyumba ya Mungu, pamoja nami na nusu ya viongozi;
41hata na makuhani waliokuwa na baragumu: Eliakimu, Maseya, Miniamini, Mikaya, Eliyoenayi, Zakaria na Hanania.
42Hao walifuatwa na Maseya, Semaya, Eleazari, Uzi, Yehohanani, Malkiya, Elamu na Ezeri. Waimbaji waliimba wakiongozwa na Yesirahia.
43Siku hiyo, watu wakatoa sadaka nyingi na kufurahi maana Mungu aliwafanya kuwa na furaha kubwa. Vilevile wanawake na watoto, wote wakafurahi. Vigelegele vya furaha toka katika Yerusalema vikasikilika mbali.
Matoleo ya ibada katika hekalu44Wakati ule wakachagua watu wa kuchunga vyumba vya gala ambamo matoleo kwa ajili ya hekalu yaliwekwa, malimbuko ya kwanza, zaka na kuyakusanya kutoka katika mashamba ya miji, kwa ajili ya makuhani na Walawi kama ilivyotakiwa na Sheria. Watu wote wakafurahia makuhani na Walawi waliotumika,
45kwa sababu walifanya ibada ya Mungu wao na ibada ya utakaso, kama vile waimbaji walivyoimba hata walinzi wa milango kulingana na agizo la mufalme Daudi na mwana wake Solomono. Ang. 1 Sik 25.1-8; 26.12
46Tangu wakati wa mufalme Daudi na Asafu kulikuwa kiongozi wa waimbaji, na kulikuwa nyimbo za sifa na shukrani kwa Mungu.
47Watu wote wa Israeli, tangu wakati wa Zerubabeli na Nehemia, walitoa matoleo ya kila siku kwa ajili ya waimbaji na walinzi wa milango. Zaidi ya yote, watu wa Israeli wakatoa matoleo kwa ajili ya Walawi, nao Walawi wakatenga sehemu kwa ajili ya wazao wa Haruni.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.