Zaburi 126 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Kuomba nguvu mupya

1Wimbo wa safari za kidini.

Yawe alipoturudisha tena Sayuni,

tulikuwa kama watu wanaoota ndoto!

2Hapo kinywa chetu kilijaa kicheko;

tulishangilia kwa furaha.

Nao watu wa mataifa mengine walisema:

“Yawe amewatendea mambo makubwa!”

3Kweli Yawe alitutendea maajabu,

tulifurahi kweli kweli!

4Ee Yawe, utengeneze hali yetu,

kama vile maji yanavyorudi katika jangwa la Negebu.

5Wanaopanda kwa machozi,

watavuna kwa shangwe.

6Wanaokwenda kupanda mbegu wakilia,

watarudi kwa furaha wakichukua mavuno.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help