Zaburi 61 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Kuomba ulinzi

1Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa vyombo vyenye nyuzi. Zaburi ya Daudi.

2Usikie kilio changu,

ee Mungu,

usikilize maombi yangu.

3Ninakulilia kutoka miisho ya dunia,

nikikuwa nimevunjika moyo.

Uniongoze juu kwenye mulima ambako siwezi kujifikisha.

4Wewe ndiwe kimbilio langu,

boma langu lenye nguvu la kukimbilia waadui.

5Ninaomba nikae katika nyumba yako milele,

nipate kukimbilia chini ya mabawa yako.

6Ee Mungu, umesikia viapo vyangu,

umenijalia sehemu yangu unayowapa wale wanaokuabudu.

7Umujalie mufalme maisha marefu,

miaka yake ikuwe ya vizazi vingi.

8Atawale milele mbele yako, ee Mungu;

wema na uaminifu wako vimulinde.

9Hivyo nitakuimbia nyimbo za sifa,

nikitimiza viapo vyangu kila siku.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help