1Yawe akamwambia Musa: Ang. Kut 25.31-40; 37.17-24
2Umwambie Haruni kwamba wakati atakapoweka zile taa saba kwenye kinara, azipange kusudi ziangaze upande wa mbele wa kinara hicho.
3Haruni akatii maagizo hayo, akaweka taa hizo kusudi ziangaze upande wa mbele wa kinara, kama vile Yawe alivyomwamuru Musa.
4Toka sehemu za juu mpaka chini kinara hicho cha taa kilikuwa kimetengenezwa kwa ufundi mukubwa kwa zahabu iliyofuliwa kufuatana na mufano ambao Yawe alikuwa amemwonyesha Musa.
Kutakaswa kwa Walawi5Tena Yawe akamwambia Musa:
6Uwatenge Walawi kutoka Waisraeli na kuwatakasa.
7Hivi ndivyo utakavyowatakasa: uwanyunyizie maji ya utakaso kisha uwaambie wajinyoe mwili muzima, wafue nguo zao na kujitakasa.
8Kisha watatwaa mwana-ngombe dume mumoja pamoja na sadaka yake ya vyakula, ni kusema unga laini uliochanganywa na mafuta; nawe utatwaa mwana-ngombe dume wingine kwa ajili ya zambi.
9Kisha utawakusanya watu wote wa Israeli na kuwaleta Walawi mbele ya hema la mukutano.
10Utakapowaleta Walawi mbele yangu, Waisraeli watawawekea Walawi mikono.
11Halafu Haruni atawaweka hao mbele yangu kama sadaka ya kutikiswa kutoka kwa Waisraeli wanitumikie.
12Kisha Walawi wataweka mikono yao juu ya vichwa vya ngombe dume hao; mumoja wao utamutoa kuwa sadaka kwa ajili ya zambi, na huyo mwingine utamutoa kuwa sadaka ya kuteketezwa inayotolewa kwangu, kwa kuwafanyia Walawi upatanisho.
13Kisha utawasimamisha Walawi mbele ya Haruni na wana wake na kuwaweka mbele yangu kama vile sadaka ya kutikiswa.
14Hivi ndivyo utakavyowatenga Walawi kati ya Waisraeli wengine kusudi wakuwe wangu.
15Kisha kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama vile sadaka ya kutikiswa wataingia kwa kutumika katika hema la mukutano.
16Hao wametolewa wakuwe wangu kabisa, pahali pa wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli.
17Maana wazaliwa wote wa kwanza kati ya Waisraeli ni wangu, wanadamu na nyama; maana niliwatakasa kwa ajili yangu siku nilipowaua wazaliwa wote wa kwanza katika inchi ya Misri. Ang. Kut 13.2
18Sasa ninawatwaa Walawi pahali pa wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli,
19na nimewatoa kwa Haruni na wana wake, kama vile zawadi kutoka kwa Waisraeli, kusudi wafanye kazi katika hema la mukutano kwa ajili ya Waisraeli na kuwafanyia upatanisho kusudi kusitokee pigo kati ya Waisraeli wakikaribia Pahali Patakatifu.
20Kwa hiyo Musa, Haruni na Waisraeli wote pamoja wakatakasa Walawi, kama vile Yawe alivyomwamuru Musa.
21Walawi wakajitakasa zambi na kufua nguo zao, naye Haruni akawatoa kama vile sadaka ya kutikiswa mbele ya Yawe. Vilevile, Haruni akafanya upatanisho kwa ajili yao kwa kuwatakasa.
22Kisha hayo Walawi wakaingia na kufanya kazi yao katika hema la mukutano chini ya usimamizi wa Haruni na wana wake, kama vile Yawe alivyomwamuru Musa.
23Yawe akamwambia Musa:
24Kila Mulawi mwenye umri wa miaka makumi mbili na mitano na zaidi, atatumika katika hema la mukutano.
25Na tangu umri wa miaka makumi tano ataacha kazi; asitumike tena.
26Lakini, anaweza kuwasaidia Walawi wenzake wanapotumika katika hema, lakini haruhusiwi kufanya kazi yoyote peke yake. Ndivyo utakavyowapangia Walawi kazi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.