Zaburi 108 - Swahili Congo Revised Bible 2002

Maombi ya kujikinga na waadui(Zab 57.7-11; 60.5-12)

1Zaburi ya Daudi: Wimbo.

2Moyo wangu ni tayari, ee Mungu.

Moyo wangu ni tayari.

Nitaimba na kukushangilia!

Amuka, ee nafsi yangu!

3Muamuke, enyi kinubi na zeze!

Nitaamusha mapambazuko!

4Ee Yawe, nitakushukuru kati ya mataifa;

nitakuimbia sifa kati ya mataifa.

5Wema wako ni mukubwa kuliko mbingu;

uaminifu wako unaenea hata kwenye mawingu.

6Utukuzwe, ee Mungu, juu ya mbingu!

Utukufu wako uenee katika dunia yote!

7Ukomboe watu hao unaowapenda;

utusaidie kwa mukono wako na kutusikiliza.

8Mungu amesema toka hekalu lake takatifu:

“Sasa nitakwenda kwa shangwe kugawanya Sekemu,

bonde la Sukoti nitalipima sehemu sehemu.

9Gileadi ni yangu na Manase ni yangu;

Efuraimu ni kofia yangu ya chuma,

na Yuda ni fimbo yangu ya kifalme.

10Moabu ni kama bakuli langu la kunawia;

nitatupia kiatu changu katika Edomu kwa kuirizi,

nitapiga kelele la ushindi juu ya Wafilistini!”

11Ni nani atakayenipeleka katika muji unaozungukwa na kuta?

Ni nani atakayeniongoza mpaka Edomu?

12Ee Mungu, umetuacha kabisa?

Wewe hauendi tena na makundi yetu ya waaskari!

13Utupatie musaada juu ya waadui zetu,

maana musaada wa mwanadamu haufai kitu.

14Mungu akikuwa upande wetu, tutashinda.

Yeye ndiye atakayewaponda waadui zetu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help